Friday, July 19

Tolu wa Dunia Alipokutana na Mtu Mfupi wa Dunia.

Wanaume hao wawili wanaoshikilia rekodi za dunia za kitabu cha Guinness, walikutana kwa mara ya kwanza katika ufunguzi wa mashindano ya wazi ya kuvunja rekodi za dunia yaliyofunguliwa nchini Uturuki.

Mturuki Sultan Kosen mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwa urefu wake wa mita 2.46 ndiye mtu mrefu kuliko wote duniani alikutana na Mchina He Pingping mwenye umri wa miaka 21 ambaye yeye urefu wake ni sentimeta 74 tu.

"Nilikuwa nikisubiria kwa hamu kukutana na Pingping tangia nilipotambulishwa rasmi kama mtu mrefu kuliko wote duniani, nimefurahi amkuja Uturuki kwenye ufunguzi wa mashindano haya ya Guinness World Records Live,", alisema Kosen.

"Nasubiria kwa hamu kumtembeza auone mji wetu mzuri wa Istanbul".

Mashindano ya The Guinness World Records live yanafanyika katika shopping Mall kubwa kuliko yote barani ulaya la "Forum Istanbul" ambapo wakazi wa Istanbul wanapewa nafasi ya kujitokeza na kujaribu kuandika majina yao kwenye rekodi za dunia.

Baada ya wiki sita katika jiji la Istanbul, mashindano hayo yatahamishiwa katika miji mingine saba ya Uturuki.

Pingping toka China ufupi wake unatokana na ugonjwa unaojulikana kama "Primordial Dwarfism" ambapo kwa mujibu wa baba yake alipozaliwa alikuwa na umbile dogo sana kiasi cha kujaa kwenye viganja vya baba yake.

Kosen kwa upande wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pituitary gigantism ambapo alikuwa na uvimbe uliomsababishia aendelee kukua muda wote, Baada ya operesheni kadhaa za kuuondoa uvimbe huo, Kosen aliacha kukua mwaka 2008.

Mbali ya rekodi ya kuwa mtu mrefu kuliko wote duniani, Kosen pia anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa na mikono na miguu mikubwa kuliko watu wote duniani.

Chini ni VIDEO na Picha za tukio la kukutana kwa Tolu wa dunia na mtu mfupi kuliko wote duniani.