Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Tuesday, July 30

Urithi wa Dunia yetu.


Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO.
Hadi mwisho wa mwaka 2009 sehemu 890 katika nchi 148 zimekubaliwa. Nchi inayoongoza kwa wingi wa mahali ni Italia yenye 45.
Orodha rasmi ya UNESCO ina mahali 689 pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali 176 pa urithi wa dunia wa kimazingira, mbali ya 25 pa mseto.
Mwanzo wa jitihada za kuhifadhi urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ilihekalu la Abu Simbel liweze kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa.
Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi ya urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira.
Kila mahali panapopendekezwa ili pakubaliwe panahitaji angalau sifa moja kati ya sita zifuatazo:
  • kuwa na thamani ya pekee ya kisanii
  • kuwa na athira muhimu katika eneo fulani au kipindi cha historia
  • kuwa kitu cha pekee kisichopatikana tena au kuwa na umri mkubwa
  • kuwa mfano bora wa kipindi fulani cha historia ya ujenzi
  • kuwa muhimu katika uhusiano na fikra muhimu au watu muhimu wa historia
Kamati ya Urithi wa Dunia hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya.

Tuesday, July 16

Mapambano kati ya polisi na waandamanaji mjini Cairo.

Maafisa  nchini  Misri  wamesema  leo  kuwa  watu  saba wameuwawa  na  wengine  261  wamejeruhiwa  katika  mapambano kati  ya  polisi  na  waandamanaji  mjini  Cairo  jana. Waandamanaji hao wamepambana  na  polisi jana na leo asubuhi  mjini  Cairo , baada  ya  waungaji  mkono  wa  rais  aliyeondolewa  madarakani Mohammed  Morsi  walipojaribu  kuzuwia  njia  muhimu  ya  darajani katika  mto  Nile. Waandamanaji , wengi  wao  vijana , waliwarushia mawe  polisi  na  kuimba  nyimbo  za  kumsifu  Morsi, wakati  polisi wakifyatua  mabomu  ya  kutoa  machozi  na  risasi  za  mipira. Morsi  aliondolewa  madarakani   na  jeshi   Julai 3,  kufuatia maandamano  ya  nchi  nzima  ambapo  waandamanaji  walikuwa wanadai  ajiuzulu.  Farid  Ismail  msemaji  wa  chama  cha  Udugu wa  Kiislamu,  amesema  kuwa  Marekani  inaunga  mkono  moja kwa  moja  kuondolewa  kwa  rais  Morsi. Wakati  huo  huo  naibu waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani  William Burns ametaka kufanyike  majadiliano  zaidi nchini  humo.
O-Ton  William Burns
Naibu  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani  William  Burns amekuwa  afisa  wa  ngazi  ya  juu  wa   nchi  hiyo  kufanya  ziara nchini  Misri  tangu  kuondolewa  madarakani  kwa  rais Morsi . Burns amekosoa  hatua  ya  waendesha  mashtaka  wa  serikali kuwakamata  viongozi  waandamizi  wa  kundi  la  Udugu  wa Kiislamu.