Showing posts with label Tenisi. Show all posts
Showing posts with label Tenisi. Show all posts

Tuesday, September 10

Rafael Nadal bingwa US open

Rafael Nadal amemcharaza bingwa wa dunia wa tennis ya wanaume Novak Djokovic kwenye mchuano wa fainali ya shindano la US open mjini New York Marekani na ambalo amelishinda kwa mara ya pili.
Mchuano huo wa seti nne ulikuwa mkali sana.

Nadal raia wa Uhispania na mwenye umri wa miaka 27, alicheza vyema sana na kushinda mchuano kwa 6-2 3-6 6-4 6-1 katika muda wa saa tatu na dakika ishirini na moja.

Nadal sasa ameshinda mashindano 13 makubwa ya Grand Slam na kusemekana kuwa mchezaji pekee anayeweza kumkaribia aliyekuwa bingwa wa tennis Pete Sampras.
Na baada ya kukosa kushiriki michuano ya US Open mwaka jana kutokana na jeraha, Nadal sasa anajiandaa kuchukua nafasi ya kuwa mchezaji nambari moja wa Tennis duniani.

"ushindi wangu umenifurahisha sana,'' alisema Nadal akiongeza kuwa hakutarajia kushinda. ''Hivyo ndivyo maisha yalivyo, na nina bahati sana.''
"napenda sana ushindani na pia napenda sana mchezo huu. Maisha yangu yote nimekuwa nikiota kuhusika na mashindano kama haya.

Chanzo: bbc

Monday, September 9

Serena Williams atwaa Combe la US Open 2013

Bingwa wa dunia wa Tenis kwa wanawake, Serena Williams ameshinda kwa mara ya kumi na saba shindano la US Open, katika fainali lliyokuwa yenye mbwembwe dhidi ya Victoria Azarenka katika uwanja wa Flushing Meadows.

Serena mwenye umri wa miaka 31, aliweza kuibuka mshindi dhidi ya Azarenka kwa kumshinda kwa seti tatu kati ya nne na hivyo kupata ushindi kwa mara nyingine.
Williams sasa ameshinda shindano hilo kwa mara ya kumi na saba.
Lakini baada ya ushindani mkali kutoka kwa Azarenka, Williams alilazimika kujitahidi zaidi ya alivyokuwa anacheza ili aweweze kupata ushindi kama ilivyokuwa katika michezo mingine 16 iliyopita ambapo aliweza kushinda.

Azarenka, mwenye umri wa miaka 24, aliwahi kumshinda Williams mara mbili mwaka huu , mara ya mwisho kwenye mchezo uliochezwa wa kirafiki eneo la Cincinnati mkesha wa shindano la US Open, mwaka huu na kujiamini kuwa angeweza kumshinda mmarekani kwenye ukumbi mkubwa.
Williams alionekana kuwa katika hali nzuri wakati wa shindano lote.

Chanzo: bbc

Monday, July 8

Murray bingwa mpya wa Wimbledon



Andy Murray amekuwa Muingereza wa kwanza kushinda taji la Wimbledon tangu mwaka 1936, ikiwa ni zaidi ya miaka 77.
Murray amemfunga Novak Djokovic raia wa Serbia kwa seti tatu kwa kwa bila katika mchezo wa fainal za wanaume za michuano ya tenesi ya Wimbledon.
Murray amemshinda mchezaji anayeorodheshwa wa kwanza duniani Novak Djokovic kwa seti tatu kwa bila za 6-4, 7-5, 6-4.
Andy Murray amesema anashindwa kuamini kile alichokifanya kwani mechi hiyo ilikuwa ngumu, huku joto likiwa kubwa lakini anashukuru ameweza kumaliza mechi hiyo kwa ushindi muhimu kwake na kwa taifa.
Hili ni taji la pili la michuano mikubwa ya tenesi duniani maarufu kama Grand Slam baada ya kushinda lile la Michuano ya wazi ya Marekani.
Muingereza wa mwisho kushinda taji la Wimbeldon ambalo hufanyika mjini London kila mwaka alikuwa ni Fred Perry aliyeshinda taji hilo kwenye michuano ya mwaka 1936.
Mwaka jana Andy Murray alipoteza mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon kwa kufungwa na Roger Federer.
Malkia wa Uingereza, Elizabeth wa pili amemtumia ujumbe wa Pongezi Andy Murray kwa ushindi wake katika mechi ambayo ilishudiwa pia na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon.

BBC.