Showing posts with label Mazingira. Show all posts
Showing posts with label Mazingira. Show all posts

Thursday, June 20

Mafuriko yatishia kupindukia yale mwaka 2002

Kansela Angela Merkel ameyatembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko makubwa kusini na mashariki ya Ujerumani katika wakati ambapo kima cha maji kinazidi kupanda katika baadhi ya maeneo ya Ulaya ya kati .
Hali bado ni ya wasi wasi nchini Ujerumani,jamhuri ya Tcheki ambako mtu wa nane amegunduliwa amekufa ,pamoja pia na Austria,walikokufa watu wawili,Uswisi mtu mmoja na Hungary.
Kote huko mafuriko yamesababisha maafa na hasara kubwa na maelfu ya watu kulazimika kuzihama nyumba zao.
Kansela Angela Merkel, akivalia koti jeusi na viatu vya mvua,aliutembelea mji wa Passau,katika jimbo la kusini la Bavaria,mmojawapo ya miji iliyoathirika zaidi na mafuriko hayo.Kansela Angela Merkel ameahidi msaada wa dharura wa Euro milioni 100 kuyasaidia maeneo yaliyoathirika.Kansela Angela Merkel amesema:
Kansela Angela Merkel amepanga kuitembelea miji mengine pia iliyoathirika katika jimbo la Saxony na Thüringen ambako kima cha maji kinazidi kupanda.Wanajeshi elfu nne wamepelekwa kusaidia.
Duru zinasema hata hivyo katika mji wa Passau ambako maji ya mito mitatu inamwaagikia katika mto Danube,kima cha maji kimeanza kushuka.

Bado hali si shuwari

Mjini Prague,maji ya mto Valtva yamefikia kilele chake i na maji yanaayofurika yanaelekea kaskazini ya jamhuri ya Tcheki.
Wasi wasi mkubwa zaidi ni katika mji wa Usti-nad-Labern,mji wa kiviwanda wenye wakaazi laki moja unaokutikana karibu na mto Elbe,kilomita 30 karibu na mpaka wa Ujerumani.
Viwanda vya kemia katika eneo hilo vimefungwa,viongozi wakihofia waasije wakashuhudia balaa kama lile lililotokea katika mafuriko ya mwaka 2002 .
Nchini Austria kima cha maji ya mto Danube kinatarajiwa kupanda wakati wowote ule na kufikia kiwango sawa na kile cha mafuriko ya mwaka 2002.
Nchini Hungary waziri mkuu Viktor Urban ametangaza hali ya hatari katika baadhi ya majimbo kutokana na kuzidi kupanda kima cha maji ya mto Danube.Na huko pia wanajeshi elfu nane pamoja na maelfu ya waokozi na askari polisi wamepelekwa katika maeneo ya maafa.

DW.

Thursday, May 9

Wasiwasi waongezeka huku mafuriko yakiharibu miji ya Somalia

Mvua kubwa mno katika wiki za hivi karibuni zimesababisha mto Shabelle kuvunja kingo zake kwenye mikoa ya Somalia ya Hiran, Shabelle ya Kati na Shabelle ya Chini, ikiwaacha mamia ya familia kukosa makazi na kuhitaji sana usaidizi kutoka wakala wa misaada wa kitaifa na kimataifa kusaidia.Gavana wa Hiran Abdi Farah Laqanyo alisema mwitikio wa ukoaji wa taratibu kwenye mafuriko umechanganya utawala wake, na kutuhumu asasi za kitaifa na kimataifa kwa kupuuza hali ya hatari ya kibinadamu inayokabili mamia ya familia ambazo zilikimbilia maeneo ya karibu na Beledweyne.
"Ninatoa wito kwa [mashirika] kuchukua hatua katika hali ya kibinadamu kusaidia wale walioathiriwa vibaya na kukosa makazi, kwa sababu mvua na mito iliyofurika imeingilia harakati za watu katika maeneo ya makazi ya jiji hilo, ambalo limezungukwa na nyanda zenye miamba," aliiambia Sabahi.
"Wenyeji pia wanapata ugumu kwenda kununua vitu, kwani maji yanasomba lundo la matope, uchafu na mwamba kwenye makazi na kwenye mitaa yaliyoharibika, hali inayosababisha kuenea kwa hali kama vile kipindupindu mbaya, malaria na utapiamlo," alisema.
Mabwawa mengi kandokando ya Mto Shabelle yalishindwa au kuharibika kisasi cha kushindwa kutengenezwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 1991, gavana huyo alisema. Mafuriko yameharibu maisha ya wananchi na kuharibu mazao, nyumba na majengo madogomadogo, wakati magonjwa ya kuambukiza, utapia mlo na umaskini imewakumba wanakijiji.
Gavana wa Shabelle ya Chini Abdiqadir Mohamed Nur alisema mvua na mafuriko zimeharibu makazi kadhaa huko Janaale na Wanlaweyn, na kuharibu mali na kuwafanya wamiliki kuhama pasipo kutarajia. Wakaazi wamekimbilia kwenye manispaa na mashirika ya misaada kwa ajili ya kusaidia na huduma za afya, kwani maji machafu yanayotoka majumbani yamechanganyikana na maji ya mafuriko na kusababisha mgogoro wa afya ya umma, alisema.
Mafuriko ya Mto Shabelle yamefanya mji wa Beledweyne kutoendelea na chochote na kusomba dazeni za vijiji, migomba na mashamba ya nafaka. Watoto wanne wamekufa mjini hapo, alisema.
"Tumeorodhesha ajali za barabarani na kuanguka kwa majengo mengi kwani mafuriko yamewatisha wakaazi ambao wamekuwa wakiagiza makazi bora mara kadhaa kabla ya msiba wa msimu huu kwa sababu walijua majengo machakavu hayatahimili," Nur aliiambia Sabahi.

Miji yageuka kuwa vinamasi


Deqa Nurani Said, mama mwenye watoto nane mwenye umri wa miaka 32 huko Wanlaweyn, alisema alijihifadhi katika shule ya msingi ya umma, lakini mamia ya wakaazi wengine walikuwa wakilala katika eneo la wazi, karibu na barabara kuu. Hakuna shirika lililowapa msaada na huduma za uokozi au msaada wa matibabu, au kujaribu kusaidia familia zilizoathirika,alisema.
"Tunakabiliwa na hatari ya njaa na magonjwa na joto viko chini sana," aliiambia Sabahi. "Mvua imeendelea kunyesha sana katika wiki chache zilizopita. Mamia ya wakaazi wamelazimishwa kuhama nyumba zao, kwani mafuriko yamesomba nyumba zote na maghala mjini, ambako hakuna miinuko yoyote ya kuwaokoa dhidi ya maji ya mafuriko yanayosambaa. Hatujaona pia operesheni yoyote ya kutoa maji au ujenzi mpya wa kingo za mito"
Gavana wa Shabelle ya Kati Abdi Jinow Alasow alisema mafuriko yamewalazimisha wakaazi huko Jowhar kukimbia usiku baada ya maji kusomba vibanda vyao. Mafuriko pia yamekata barabara, njia za simu na umeme, kuwatenganisha wakaazi katika vitongoji vyao.
Alasow alisema mamia ya familia zinaishi mitaani. Maisha huko Jowhar yamesimama katika sekta nyingi muhimu, alisema, maji taka yamefurika kwa sababu hakuna njia za maji taka.
"Mji wa Jowhar, ambao unajulikana sana kwa kilimo cha mpunga na mbogamboga, umekuwa na usiku wa kusikitisha kutokana na mvua kubwa, ambazo zimesomba mto," aliiambia Sabahi. "Jiji halijawahi kuona mvua nyingi kama hiyo. Saa nane za mafuriko zilitosha kubomoa mitaa yote ya mji mkongwe, kugeuza baadhi kuwa vinamasi."
SABAHI ONLINE.

Wednesday, March 20

Usafi wa mazingira katika nchi zinazoendelea


Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanajumuisha lengo la kupunguza kwa takribani nusu nambari ya watu ambao hawana usafi wa mazingira ifikapo mwaka 2015. Mnamo Desemba 2006, Baraza la Umoja wa Mataifa katika mukutano wao ilitangaza Mwaka wa 2008 kuwa 'Mwaka wa Kimataifa wa Usafi wa Mazingira, kutambua upole wa utendekezaji wa Lengo la Maendeleo ya Milenea la (MDGs) la usafi wa mazingira. Mwaka huo ulilenga kuendeleza ufahamishaji na vitendo ili kufikia hayo malengo. Haya ilifanywa hasa katika:
  • Kuondoa unyanyapaa wa usafi wa mazingira, ili kuwezesha majadiliano ya umuhimu wa usafi wa mazingira.
  • Kubainisha upunguzaji wa

Friday, February 15

Historia Ya Usafi wa Mazingira

Usafi wa mazingira ni muhimu kwa afya zetu.
Ushahidi wa usafi wa mazingira mijini ulionekana mara ya kwanza katika miji ya Harappa, Mohenjo-daro na hivi karibuni Rakhigarhi ya majimbo yaliyoendelea bondeni la Indus wakati wa ustaarabu. Mipangilio hiyo ya miji ilizingatia mifumo ya kwanza ya usafi wa mazingira mijini. Ndani ya mji, nyumba au vikundi vya nyumba yalipata maji kutoka visima. Kutoka ndani ya chumba kilicho kuwa kimetengwa kwa ajili ya kuoga, maji taka ilielekezwa chini ya mitaro iliyofunikwa kando ya barabara kuu. Manyumba yalifunguka tu kwa mabehewa ya ndani na makoboti madogo.
Miji ya Kirumi ilikuwa na vipengele vya mifumo ya usafi wa mazingira, yakutoa maji katika mitaa ya miji kama vile Pompeii, mawe ya ujenzi na mbao za kukusanya na kuondoa maji machafu kutoka maeneo ya wakazi - kwa mfano maxima Cloaca katika mto Tiber Roma . Pia kuna rekodi za usafi wa mazingira mahala pengine katika Ulaya mpaka wakati wa

Wednesday, February 13

Utunzaji wa mazingira ni muhimu.

Mazingira ukiyatunza, nayo yatakutunza

Akizungumza katika mkutano wa siku moja, uliofanyika uwanja wa Gombani Pemba, Afisa Elimu ya mazingira kutoka Idara hiyo, Hamza Rijali alisema suala la kuhifadhi mazingira haliihusu Idara hiyo pekee, bali kila mmoja.

Alisema, utunzaji na uhifadhi wa mazingira ni suala pana kuliko linavyofikiriwa, na ndio maa Idara hiyo ya Mazingira, ikaamua kuwaita wadau wake mbali mbali ili kutoa mawazo na fikra zao katika kuuimarisha mpango huo mkakati.

Rijali alieleza kuwa, mpango huo hautokamlimilika vyema na kufanikiwa kuutekelezwa pasi na wadau na wao kutoa mchango, ambao anaamini utasaidia sana ndani ya Idara ya Mazingira katika kufikia lengo lake.

‘’Kila jambo linalofanywa na Idara ya Mazingira, hasa la kuhaulisha mazingira yetu, linahitaji mikono mingi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari, Idara ya ardhi, waalimu, viongozi wa dini na hata wananchi wa

Friday, February 8

Jinsi ya kutunza mazingira yetu



 Magonjwa mbali mbali yatokanayo na mzagao wa takataka katika mazingira ya jiji la Dar es Salaam ni tishio kwa walio wengi hasa wakazi wa maeneo yanayohusiana na biashara za vyakula na maji ukiachilia mbali  matunda  ambayo  wengi huyatumia bila kujua kuwa yapo katika hali gani za usalama kwa afya zao.
Matunda hayo yanayouzwa na wenzetu katika kujitafutia riziki zao za kila siku ni chanzo cha kuibuka kwa magonjwa yanayowasumbua wenzetu katika hospitali nyingi, hasa magonjwa ya tumbo ambayo wengi wetu wakiugua hawafanyi kingine ila kununua dawa katika maduka ya dawa yaliyo karibu na makazi yao na kukuta wakati mwingine wanajiongezea matatizo ya afya zao bila kujua kile wanachoki fanya kwa dhana kwamba wanajitibu ama wanakula dawa ili wapone.
Licha ya