Wednesday, February 13

Utunzaji wa mazingira ni muhimu.

Mazingira ukiyatunza, nayo yatakutunza

Akizungumza katika mkutano wa siku moja, uliofanyika uwanja wa Gombani Pemba, Afisa Elimu ya mazingira kutoka Idara hiyo, Hamza Rijali alisema suala la kuhifadhi mazingira haliihusu Idara hiyo pekee, bali kila mmoja.

Alisema, utunzaji na uhifadhi wa mazingira ni suala pana kuliko linavyofikiriwa, na ndio maa Idara hiyo ya Mazingira, ikaamua kuwaita wadau wake mbali mbali ili kutoa mawazo na fikra zao katika kuuimarisha mpango huo mkakati.

Rijali alieleza kuwa, mpango huo hautokamlimilika vyema na kufanikiwa kuutekelezwa pasi na wadau na wao kutoa mchango, ambao anaamini utasaidia sana ndani ya Idara ya Mazingira katika kufikia lengo lake.

‘’Kila jambo linalofanywa na Idara ya Mazingira, hasa la kuhaulisha mazingira yetu, linahitaji mikono mingi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari, Idara ya ardhi, waalimu, viongozi wa dini na hata wananchi wa
kawaida’’,alieleza Mtaalamu huyo wa mazingira.

Katika hatua nyengine alisema, Idara hiyo ya Mazingira ilkaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na mpango mkakati, na ilikuwa ikijiendesha katika mazingira yasio mazuri, mbapo kwa sasa kukamilika kwa mpango huo itakuwa na dira.

Kwa upande wake muwezeshaji katika kufanikisha mpango huo, Mark Joffre kutoka mji wa Norrich nchini Uengereza, alisema kutokana na udogo wa visiwa vya Zanzibar, ni rahisi sana kutunza na kuhifadhi mazingira iwapo jamii itaisaidia Idara husika.

‘’Jamii isiiachie Idara ya Mazingira pekee ,maana wao watendaji ni kidogo, lakini jamii ni kubwa na wanatumia mazingira kwa kazi zao za kila siku, sasa ipate taarifa kutoka kwenu ili ikamalishe vyema kazi zake’’,alifafanua Mark.

Hata hivyo aliitaka Idara ya Mazingira, kuzitumia sheria na kanuni zilizopo ili jamii ipate woga wa kuharibu na kuchafua mazingira, kwani bila ya sheria kufuatwa suala la uharibifu litaendelea.


Wakichangia mpango huo mkakati washiriki wa mkutano huo, waliomba Idara ya Mazingira kuhakikisha makundi maalum ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu kupewa kipaumbele katika uhifadhi na utunzaji mazingira.

Aidha walipendekeza kuwa vyombo vya habari, vitumike ili kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabonanza ili kuona suala la uhifadhi mazingira limo kwa wingi vichwani mwa jamii.

Katika mkutano huo wa kuuchangia ‘mpango mkakati’ wa Idara ya Mazingira kwa miaka mitano ijayo, wadau kutokana Idara za vitegu uchumi, habari, kilimo, mazingira, watu wa kawaida walihudhuria.