Showing posts with label Soka. Show all posts
Showing posts with label Soka. Show all posts

Tuesday, October 8

Herve Renard aaga Chipolopolo.

Zambia imempa idhini kocha Herve Renard kuyaacha majuku yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo ili kuchukua jukumu lake jipya la kuwa kocha wa timu ya ufaransa ya FC Sochaux.
Kocha huyo alikuwa ameanza muhula wa pili wa mkataba wake kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mnamo mwezi Oktoba mwaka 2011 na kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika miezi minne baadaye.
Lakini Zambia ilikuwa na wakati mgumu mwaka huu kiaso cha kubanduliwa nje ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Zambia sasa imempa kazi ya muda Patrice Beaumelle kuwa kocha wa Chipolopolo.
Beaumelle, amekuwa akifanya kazi kama kocha wa muda, na atashikilia wadhifa wa kocha mkuu wakati Chipolopolo watapocheza mechi ya kirafiki na Brazil mjini Beijing tarehe 15 Oktoba.
Shirikisho la soka nchini humo katika taarifa yake lilisema kuwa kocha "Herve Renard ameachishwa majuku yake ili kumruhusu kuiongoza timu ya Ufaransa.''

Renard, mwenye umri wa miaka 45, alichukua wadhifa huo wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2008 na aliiongoza timu hiyo hadi kufika robo fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Baadeya alikuwa kocha wa timu ya Angola na USM Alger kwa muda kabla ya kurejea kuwa kocha wa Zambia na kutimiza ndoto yake ya kuiongoza Zambia kunyakua kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2012.

Chanzo: bbc

Thursday, September 12

Shola Ameob Afurahia.

Mchezaji soka Mnigeria Shola Ameobi amesema kuwa ana furaha isiyo na kifani kwa kuingiza bao lake la kwanza katika mechi ya kitaifa na ya kirafiki kati ya Nigeria na Burkina Faso ambapo Nigeria ilishinda kwa mabao 4-1 .
Mchezaji huyo anayechezea Newcastle aliambia BBC kuwa , hatimaye ameingiza bao na kuwa ana furaha sana .
''Ilinichukua muda lakini pindi nilipoupata mpira , niliweza kujitahidi kuinguiza bao. Nimekuwa kwa muda murefu nikitaka kuingiza bao hilo, hilo lilipofanyika, nilihisi kama nimetimiza ndoto yangu,'' alisema Shola

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya kitaifa ya vijana Uingereza, alikubaliwa tu mwaka jana Novemba kuchezea Super Eagles, na hadi kufikia sasa, amecheza mara nne, anatumai kuwa kuanzia sasa ataweza kuwa kiungo muhimu kwa timu ya taifa Nigeria ambao ni mabingwa wa afrika.

Wakati huohuo, Nigeria ilimaliza ya kwanza katika kundi F kwenye michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa nchi za Afrika, kutokana na ushindi wao dhidi ya Mali ambapo walishinda kwa mabao mawili bila mwishoni mwa wiki.

Sasa wanasubiri draw ya Jumatatu kwa michuano wa mwisho ambayo itawahusisha washindi kumi wa mechi zilizopita.
Haya ndiyo matokeo ya mechi za kirafiki zilizochezwa Jumanne zikihusisha timu za Afrika.

Chanzo: bbc

Wednesday, September 11

England yatoka sare na Ukraine katika mchezo wakusaka nafasi ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Brazil.

Meneja wa timu ya Uingereza Roy Hodgson, amesema aliridhika na walivyocheza wachezaji wake walipojitosa katika michuano ya kuwania kombe la dunia.
England ilienda ilimaliza mchezo kwa sare tasa dhidi ya Ukraine kwenye mechi iliyochezwa mjini Kiev
Kikosi cha Hodgson kinasalia juu katika kikundi cha H na kitafuzu ikiwa kitashinda mechi zao mbili za kufuzu dhidi ya Montenegro na Poland zitakazochezwa katiika uwanja wa Wembley.
Baadhi ya mechi ambayo walisema ilikosa msisimuko na ambayo ilichezwa mbela ya mashabiki 70,000, meneja huyo wa England alisema, "kabla ya mchezo, hisia waliyokuwa nayo wengi ni kwamba matokeo ya sare yoyote hayatakuwa mabaya.''

England iliingia kwenye mchezo huo, bila ya wachezaji, Danny Welbeck ambaye huchezea Man U , Wayne Rooney na mshambulizi wa Liverpool Daniel Sturridge ambao hawakucheza kutokana na majeraha.
Uwezo wetu wa kushambulia ulikuwa mdogo sana kwa sababu hatukuwa na wachezaji, Rooney, Welbeck na Sturridge, alisema Hodgson.

"pia tulimpoteza kiungo cha kati, Alex Oxlade-Chamberlain kwa sababu ya jeraha la goti ingawa wachezaji waliowakilisha kwenye mchezo huo walicheza vyema.
Sare hiyo iliisongesha England mbele kwa pointi moja kwenye kundi la H ikisalia na michuano miwili.

Chanzo: bbc

Friday, September 6

Messi alipa deni.

Lionel Messi -nyota ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina pamoja na babake wamelipa euro milioni tano(sawa na dola milioni 6.6) deni la kodi kabla ya kukabiliana na mashtaka ya kukwepa kodi kwa njia za ujanja, kwa mujibu wa uwamuzi wa jaji mapema leo Alhamisi.
Madai haya ya kukwepa kodi yaliyowasilishwa mahakamani mapema mwezi juni yalikua pigo kubwa kwa hadhi ya mcheza soka huyu ambaye kabla ya hapo alionekana kama mnyenyekevu asiye mizengwe ukimlinganisha na mtani wake mkuu Cristiano Ronaldo mwenye mbwembwe.
Maamuzi ya jaji huko Gava, kwenye pwani ya bahari Mediterenian karibu na mji wa Barcelona, amesema kua babake Messi Jorge Messi alilipa euro milioni 5.02 kwenye mahakama tarehe 14 mwezi Agosti kufidia kodi inayodaiwa haikulipwa pamoja na riba.

Jaji huyo amepinga ombi la mwanasheria wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutaka alipe kwa dhamana ya hisa ili kuhakikisha kua riba yoyote itakayosababishwa na kesi inalipwa.
Jaji alisema kua haina haja kwa sababu ya uwezo alio nao Bw.Lionel Andres Messi Cuccittini akiongezea kua tayari kodi hiyo imeisha lipwa.

Suala ambalo jaji huyo amesema bado anashauriana na mwanasheria wa upande wa mashtaka ni kuhusu ombi la Messi kutaka kusikilizwa kwa kesi hiyo kuahirishwe kutoka tarehe 17 septemba.
Mashtaka dhidi ya Messi na babake Jorge ni kuhusu kuibia kodi inayotokana na mapato ya biashara zinazotumia sura yake kuanzia mwaka 2006 na 2009.

Inadaiwa kua Messi na babake walijaribu kulihadaa taifa kwa kuhamisha hati miliki za malipo hayo kwenye makampuni yaliyo nje kama huko Belize na Uruguay ili wasilipe kodi nchini Uhispania.
Mawakili wa Messi Juarez Veciana, wamesema kua mteja wao anakubaliana na sheria za Uhispania na yupo tayari kulipa kila fedha anayotakiwa kulipa.

Ufanisi wa Messi uwanjani umemfanya kua mmoja ya sura zinazouzika duniani akiwa namba 10 kwenye orodha ya Forbes miongoni mwa wana michezo mashuhuri wenye mapato makubwa akikadiriwa kupokea dola milioni 21 kila mwaka kutokana na matangazo ya biashara peke yake.

Chanzo: bbc

Monday, September 2

Mesut Ozil kutua Arsenal?

Kunako siku ya mwisho kwa vilabu vya mpira wa miguu kukamilisha usajili wa wachezaji klabu ya Arsenal imeafikiana na mchezaji Mesut Ozil wa Ujerumani anayechezea klabu ya Real Madrid kwa kitita cha pauni za Uingereza milioni £42.4.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, klabu ya Arsenal imekubaliana na Real Madrid kuilipa pauni za Uingereza milioni £42.4m sawa na Euro milioni 50 kumsajili Mjerumani Mesut Ozil.
Kijana huyo menye umri wa miaka 24 amefikia makubaliano na Arsenal kuhusu maslahi yake binafsi ingawa sharti apitie mchakato wa vipimo vya afya yake kabla ya Arsenal kukamilisha usajili ambao katika historia ya klabu hio haujawahi kufanyika kumsajili mchezaji kwa zaidi ya pauni milioni 22.

Kwa wakati huu Ozil yuko pamoja na kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani na itabidi afanyiwe vipimo huko huko Ujerumani.
Kwa kipindi cha msimu wa likizo na usajili wa wachezaji Arsenal imeshindwa kuwasajili wachezaji wa kiwango anachokitaka Arsene Wenger kama mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na Gonzalo Higuain, mchezaji mwingine aliyekua huko Real Madrid.

Lakini kwa sasa yumkini Ozil anaelekea uwanja wa Emirates kufuatia usajili wa Gareth Bale kwa kitita kikubwa cha pauni milioni 85.3.
Kabla ya kujiunga na Real Ozil alikua akichezea klabu ya Werder Bremen alikosajiliwa na Real kwa takriban pauni milioni 12.4 na kuichezea Real mara 155.

Wakati Arsenal ikijitahidi kusajili kabla ya dakika ya mwisho ya shughuli ya usajili Liverpool pia imetiliana saini na Mamadou Sakho na Tiago Ilori kwa jumla ya pauni milioni 25.
Sakho mwenye umri wa miaka 23 ameichezea Timu ya Taifa ya Ufaransa mara 14 France na amegharimu pauni milioni £18m kutoka klabu ya Paris St-Germain.

Ilori alizaliwa mjini London na ameiwakilisha Timu ya Ureno ya vijana ingawa bado anaweza kuiwakilisha England.
Liverpool haikuishia hapo ila imemzoa Mnaijeria Victor Moses kutoka Chelsea.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao 10 akishiriki mechi 42 za Cheslea lakini amekabiliwa na ushindani mkali wa kuweza kuingia uwanjani kufuatia usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil Willian, Mjerumani Schurrle pamoja na mkongwe wa Cameroon Samuel Eto'o.

Chanzo: bbc

Sunday, September 1

Hatimae Bale ampiku Ronaldo, awa mchezaji ghali duniani, atua Real Madrid.

Real Madrid imevunja rekodi ya dunia ya uhamisho wa wachezaji kwa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Gareth Bale.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ametia saini mkataba wa kuichezea Real Madrid wa miaka 6 kwa kununuliwa kitita cha pouni milioni 85,3.
Rekodi iliyokuwepo ilikuwa ya Cristiano Ronaldo aliponunuliwa na Real Madrid toka Manchester United kwa pouni milioni 80 mwaka 2009.
"nilikuwa na furaha ya miaka 6 niliyochezea Spurs,lakini huu ni wakati mwafaka kwangu kusema kwa heri "alisema Bale mwenye umri wa miaka 24.
Bale aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita katika ligi kuu ya England alijiunga na Tottenham kutoka Southampton kwa pouni milioni 10 mwaka 2007 na alifunga magoli 26 msimu uliopita.

Chanzo: bbc

Friday, August 23

Arsenal yakaribia kufuzu klabu bingwa ulaya.


Walipua mizinga wa Kaskazini mwa London, Arsenal wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya hatua ya makundi.
Arsenal iliyokuwa ugenini huko nchini Uturuki imeichapa Fenerbahce nyumbani kwao 3-0 katika mchezo ambao ulishuudia kipindi cha kwanza kikimalizika bila nyavu za timu zote kuguswa.
Pasi nzuri kutoka kwa Aron Ramsey iliyomkuta Theo Walcott ambaye bila kusita naye aliunganisha hadi kwa Kieran Gibbs aliyelitazama lango la Fenerbahce na kuandika bao la kwanza kwa Arsenal kunako dakika ya 51 ya mchezo.
Dakika chache baadaye Arsenal waliendelea kulisakama lango la Fenerbahce, lakini Aron Ramsey aliongeza matumaini ya kutopoteza mchezo wa pili na kuwapa raha mashabiki wa Ashburton Grove kwa kufunga bao la pili.

Pengine bao la pili liliwachanganya zaidi Fenerbahce ambao licha ya kucheza mechi hiyo bado wapo kwenye adhabu ya kutoshiriki michuano yoyote ya ulaya lakini rufaa waliyoikata ambayo itasikilizwa tarehe 28 mwezi wa Agosti inawafanya waruhusiwe kuendelea na mashindano.
Kinda mwiingereza Theo Walcott alikuwa mwiba kwa Fenerbahce, kwani kunako dakika ya 75 alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la kumi na nane na mwamuzi wa kati aliamuru ipigwe penati ambayo mfaransa Olivier Giroud aliipiga na kuandika bao la tatu na la mwisho kwa Arsenal.

Matoke ya mechi nyingine za kufuzu klabu bingwa ulaya, Dinamo Zagreb ilikubali kichapo cha bao 0 - 2 nyumbani kutoka kwa Austria Wien.
Ludogorets nayo ikatandikwa 2 - 4 na FC Basel ya Uswis, wakati Steaua BucureÅŸti ilitoshana nguvu na ya 1 - 1 na Legia Warszawa na Schalke 04 ya ujerumani nayo ikashindwa kutamba nyumbani baada ya kutoka sare tasa ya 1 - 1 PAOK.

Arsenal wameshiriki michuano ya klabu bingwa ulaya kwa miaka 14 mfululizo bila kukosa.
Michezo ya marudaniano itapigwa tarehe 27 Agosti.

Chanzo: bbc

Monday, August 19

Luiz Gustavo aamua kutua Wolfsburg

Vfl Wolfsburg wamefanikiwa kuinyakua saini ya mchezaji wa Bayern Munich Luiz Gustavo. Gustavo amesaini mkataba wa miaka minne na Wolfsburg na tayari amezinduliwa rasmi katika klabu hiyo
Mkataba huo unaaminika kuwa kati ya euro milioni 15 na 20. Gustavo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 alikuwa amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Arsenal. Alijiunga na Bayern akitokea Hoffenheim mnamo Januari 2011, na amaeomba kuihama klabu hiyo ili kupata nafasi ya kucheza katika timu ya kwanza kwa sababu nafasi zake za kucheza kila mara katika klabu ya Bayern zilikuwa chache msimu uliopita.

Kwingeneko Werder Bremen wamesaini mshambuliaji wa Argentina Franco Di Santom kutoka klabu ya England Wigan.
Di Santo mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na mshambuliaji wa zamani wa Bayern Nils Petersen baada ya mkataba wake na Wigan kukamilika mwishoni mwa msimu uliopita.
Katika habari yingine za Bundesliga ni kuwa kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan atakuwa mkekani kwa karibu wiki mbili baada ya kupata jeraha la mgongo wakati akiichezea timu ya taifa ya Ujerumani katikati ya wiki.

Gundogan ambaye alifunga goli la kwanza la Ujerumani katika mchuano wao dhidi ya Paraguay uliokamilika kwa sare ya kufungana mabao matatu kwa matatu, aliondolewa uwanjani katika dakika ya 26 wakati alipoanza kuhisi maumivu. Hii ina maana kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakosa mchuano wa nyumbani wa Dortmund dhidiy a Eintracht Braunschweig hapo kesho Jumapili na pia dhidi ya Werder Bremen mnamo Agosti 3.
Kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp huenda akawajumuisha kikosini wachezaji wa viungo Sven Bender na Nuri Sahin wakati pia mchezaji mpya Henrikh Mkhitaryan akitarajiwa kucheza baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu.

dw - swahili

Ubaguzi waiponza lazio.

Katika michezo sehemu ya uwanja wa klabu ya Lazio ya Italia imefungwa kwa mechi moja pekee kufuatia mashabiki kuwatusi wachezaji weusi.
wa Juve Mfaransa Paul Pogba, Kwadwo Asamoah na Angelo Ogbonna kutoka Ghana na mchezaji wa Itali mwenye asili ya Nigeria walirushiwa matusi na mashabiki kwenye uwanja wa Stadio Olimpiko mjini Roma. Hii ina maana kwamba mechi ya kwanza baina ya Lazio na Udinese katika Ligi ya Serie A itafanyika bila mashabiki uwanjani.
Kwingine hata kwa klabu za Arsenal na Fenebahce michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya ni muhimu kutokana na mapato.
Jumatano hii Arsenal iliyozongwa na matatizo inapambana na klabu inayokabiliwa na kesi mahakamani ikitishiwa kuondolewa mashindanoni.
Mawakili wa Fehnebahce wanaanza kusikiliza kesi kwa siku mbili huko Uswizi kuhusu tuhuma za ubadhirifu.
Shirikisho la UEFA liliruhusu klabu hio ishiriki mechi mbili dhidi ya Arsenal ingawa matokeo ya mahakama yanaweza yakaiondolea ushindi hata ikiwa imeshinda mechi ya nyumbani na marudiano mjini London.
Huko India maofisa wa michezo wanatokwa jasho kwa wanariadha wao kukataliwa kushiriki michezo ya Bara Asia kwa sababu ya umri wao uliozidi ule unaoruhusiwa.
Wanariadha 17 wa India wakiwa sehemu ya kikosi cha watu 27 wa India walipatikana kua na zaidi ya miaka 17 inayotakiwa kwenye mashindano haya.

Chanzo: bbc

Mourinho aanza vizuri Chelsea.

Magoli 2 yaliyofungwa katika kipindi cha kwanza,moja la Oscar na lingine la Frank Lampard yameiwezesha Chelsea kufunga Hull.
Kabla ya Chelsea kuliona lango,Lampard alikuwa amekosea mkwaju wake wa penalty uliopanguliwa na kipa Allan McGregor,lakini muda mfupi baadae Oscar akanusa nyavu kwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Kevin de Bruyne.
Lampard aliihakikishia Chelsea kuongoza na kuondoka na ushindi kwa kuingiza bao la pili.
Hull iliyopanda daraja msimu huu, juhudi zake za kujaribu kusawazisha katika kipindi cha pili hazikufua dafu baada ya walinzi wa Chelsea kuwa makini na kudhibiti sawa sawa nafasi zao.
Kwa ushindi huo wa kwanza wa Mourinho tangu aliporudi kuifundisha tena Chelsea,meneja huyo sasa anaweza kuelekeza macho yake na mbinu zake kwa mechi itakayofwatia ,Chelsea itakapoikaribisha Aston Villa jumatano.
Mapema ya hapo,Tottenham walijipatia ushindi wa goli 1 bila kwenye uwanja wa Crystal Palace kupitia mshambuliaji wao mpya Roberto Soldado aliyetikisa nyavu kunako dakika ya 50 kwa njia ya penalty.
Siku ya kwanza ya michuano ya ligi ya England inakamilika leo kwa mchuano mkali, Manchester City ikiikaribisha Newcastle.


Chanzo:bbc

Sunday, August 18

Arsenal yaangunkia pua nyumbani katika ligi kuu ya Uingereza.




Msimu wa Ligi Kuu ya soka ya England umeanza kwa kishindo kwa Aston Villa kuwashtua Arsenal kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Emirates.

Arsenal ndio waliofungua mlango katika dakika ya 6 kupitia Olivier Giroud. Lakini mabao mawili ya Christian Benteke kwa mikwaju ya penati yaliwakatisha tamaa mashabiki wa Arsenal.
Bao la tatu la Villa limefungwa na Antonio Luna.
Wengine walioshinda ugenini ni Fulham walioifunga Sunderland bao moja kwa bila na Southampton waliilaza West Bromwich pia kwa bao moja kwa bila liliofungwa na Rickie Lambert. Liverpool iliibuka na ushindi wa chupu chupu wa bao moja kwa bila dhidi ya Stoke City liliofungwa na Daniel Sturridge, goli la kwanza kufungwa msimu huu.
Mlinda lango Mignolet aliiokoa penalti katika dakika za mwisho za mchezo huo. Westham United waliwakaribisha Cardiff City katika ligi kuu kwa kuwafunga mabao mawili kwa bila. Norwich City ilitoka sare mawili kwa mawili na Everton.

Chanzo:BBC

Wednesday, August 14

Misri yaiadhibu Uganda.

Kocha wa timu ya taifa ya Misri - Bob Bradley.

Licha ya machafuko kuendelea nchini mwao, timu ya taifa ya Misri imeitandika Uganda The Cranes mabao 3-0.

Mabingwa wa kihistoria wa Afrika, wameifunga Uganda katika mchezo huo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja El Gouna kilometa 430 kutoka mji wa Cairo ambako machafuko yametokea.

Ahmed Hassan Koka ambaye anakipiga kwenye klabu ya Rio Ave ya Ureno alifunga bao la kwanza kwa Mapharao katikati ya kipindi cha kwanza.
Bao la pili lilifungwa dakika 12 baada mapumziko na mfungaji bora wa michuano ya kufuzu kombe la dunia kwa kanda ya Afrika Mohamed Salah.
Ibrahim Salah alihitimisha ushindi wa Misri kwa kufunga bao la tatu.
Misri imecheza bila wachezaji wake wa timu za Al Ahly na Zamalek ambao wanajiandaa na mechi ya raundi ya pili ya klabu bingwa barani Afrika.
Mchezo huo kwa Uganda ulikuwa ni kwaajili ya kujiandaa na mechi muhimu ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Senegal nchini Morocco mwezi ujao.
Katika Mchezo mwingine wa Kirafiki, Malawi imeichapa Rwanda 1-0 katika mchezo uliochezwa mjini Kigali.

BBC

Amanusura England waadhirike kwa Scotland.

Kijana Rickie Lambert aliookoa jahazi la Uingereza pale alipofunga bao la ushindi mara tu alipoingia uwanjani katika mpambano uliogaragazwa katika Uwanja wa Wembley.
Hii ni mechi ya kwanza kabisa kwa Lambert kuichezea Uingereza.
Awali mchezaji James Morrison aliipatia Scotland bao la mapema baada ya kuchomoa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Uingereza Joe Hart kuzuia
lakini baadae msambulizi Theo Walcott alisawazisha bao hilo baada mchezo safi .
Hata hivyo furaha ya Uingereza haikudumu kwani dakika chache baadae Kenny Miller aliiweka Scotland kifua mbele kwa mkwaju mkali ambao kipa wa Uingereza hakuoona.
Baada ya kipyenga cha mwisho mashabiki wapatao 80,000 waliinuka vitini mwa wakiwa wameridhika na jinsi maasimu hao wawili wa soka walivyosakata kabumbu.

BBC

Man United yatakata ngao ya jamii.


Manchester United yanyakua kombe la Community Shield. Robin van Persie amehakikisha kuwa meneja David Moyes ameanza kunyakua kombe kama Meneja wa Manchester United
Meneja mpya wa United Moyes alitumia muda wake mrefu katika mazungumzo juu ya hatma ya mashambuliaji Wayne Rooney,lakini uwanjani amekuwa mshambuliaji Van Persie aliyefunga magoli mengi msimu uliopita ambaye tena ameiwezesha timu hiyo kuibuka mshindi.
Mchezo ulipoanza, imemchukua dakika 6 tu Van Persie kunusa nyavu kwa kuunganisha kwa kichwa mpira uliopigwa na mlinzi wa kushoto, Patrice Evra.
Wigan ambayo sasa inacheza katika daraja la pili,imejaribu kutishia ngome ya United bila mafanikio kwani walinzi wake walionekana kudhibiti vilivyo sehemu zao uwanjani.
United walijihakikishia kuondoka na ushindi kunako dakika ya 59 ambapo pia amekuwa mshambuliaji Van Persie aliyetikisa wavu kwa mkwaju wake uliopiga kwenye mguu wa mlinzi wa Wigan na kumhadaa mlinda lango.
Ushindi huo wa Manchester United wa magoli 2-0 ametosha kwa meneja mpya David Moyes kusherehekea kombe la community Shield,kombe lake la kwanza.
Baada ya ushindi huo sasa macho yanaelekezwa upande wa ligi kuu ambapo United wataanza kampeni ya kutetea taji lao ugenini dhidi ya Swansea siku ya jumamosi.

Tuesday, July 23

Je! Man U watafanikiwa kumsajiri Cesc Fabregas?

Cesc Fabregas - Barcelona FC.
Klabu ya Barcelona imeiambia Manchester United kuwa haina nia ya kumuuza nyota wake Cesc Fabregas.
Manchester United, imethibitisha kuwa iliwasilisha tena ombi la kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni thelathini, lakini ripoti zinasema kuwa ombi hilo limekataliwa.
Rais wa Barcelona Sandro Rossel, amekariri kuwa klabu hiyo haina nia ya kumuuza mchzaji huyo kwa klabu yoyote.
Kocha wa Manchester United, David Moyes amenukuliwa akisema huenda wasifanikiwe kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo Moyes amekiri kuwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward, angali anafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa wamemsajili mchezaji huyo.
Mara ya kwanza United iliwasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Barcelona.
Siku mbili tu baada ya United kuwasilisha ombi hilo, Woodward alikatiza ziara yake nchini Australia na kurejea nyumbani kuongoza mikakati ya kumsajili Fabregas, kabla ya muda wa mwisho wa usajili kukamilika. Barcelona haijatoa taarifa yoyote, lakini kuna habari kuwa huenda matatizo yanayokumba klabu hiyo kwa sasa yamechangia pakubwa uamuzi huo kukataliwa.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Haijulikani ikiwa uamuzi wa Chelsea wa kutaka kumsajili mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney umechangia klabu hiyo kutaka kumsajili Fabregas.

BBC

Tuesday, July 16

Fabregas asema hataki kurudi England

Mcheza kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amesema hana nia yoyote ya kuihama klabu hiyo na kurejea tena nchini England.
Hayo ni kwa mujibu wa kocha wake Tito Vilanova.
Klabu ya Manchester United siku ya Jumatatu iliwasilisha ombi la kutaka kumasajili nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini Vilanova amesema mchezaji huyo anataka kusalia nchini Uhispania kwa sasa.
''Ni ishara nzuri kwa klabu yoyote kupata maombi kutoka kwa vilabu vingine, vinavyotaka kuwasajili wachezaji wake, lakini Fabregas amesema anataka kusalia'' Alisema kocha huyo.
Vilanova ameongeza kusema kuwa'' Fabregas hataki kujiunga na timu zingine kwa sababu ya pesa au kutokana na muda wake wa kucheza uliosalia. Anafahamu huku kuna ushindani mkali, lakini ni uamuzi wake kusalia na Barcelona. Kwa sasa nimetulia''.
Kufikia sasa Barcelona halijasema lolote rasmi kuhusiana na ombi hilo la Manchester United, ambalo linaaminika kuwa chini ya dhamana kamili ya mchezaji huyo.
Fabregas alikuwa mchezaji mchanga zaidi wa Arsenal wakakti aliocheza dhidi ya Rotherham United wakati wa mechi ya kombe la ligi mwaka wa 2003 akiwa na miaka kumi na saba na siku mia moja na sabini na saba.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Arsenal walioishinda timu ya Manchester United kupitia mikwaju ya penalti kwa fainali ya kombe la FA mwaka wa 2005.
Vile vile Fabregas, anaichezea timu ya taifa ya Uhispania na aliisaidia kunyakua kombe la dunia na pia kuwa mabingwa wa bara Ulaya mara mbili.
Alijiunga na Arsenal mwaka wa 2003 akiwa na umri wa miaka kumi na sita.
Fabregas aliichezea Arsenal mechi 303 na kufunga magoli 57, kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 25.4 kwa mkataba wa miaka mitano kwa wa 2011.

BBC

Uholanzi yaizuia Ujerumani michuano ya mataifa ya ulaya kwawanawake.


Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Ulaya kwa upande wa wanawake Ujerumani imeshikwa shati na Waholanzi mwanzoni mwa michuano hiyo nchini Sweden.Kocha mpya wa Bayern Munich Pep Guardiola aishutumu Barcelona .
Mabingwa watetezi Ujerumani walitoka sare ya bila kufungana na Uholanzi siku ya Alhamis katika mchezo wao wa ufunguzi katika kundi B la mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Ulaya kwa wanawake nchini Sweden. Katika mchezo mwingine wa kundi B Iceland ilipata bao la dakika za mwisho na kupata point moja muhimu katika mchezo uliotoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Norway. Hakuna timu ambayo imeweza kupata ushindi katika fainali hizi za kombe la mataifa ya Ulaya kwa wanawake hadi sasa, baada ya wenyeji Sweden kutoka sare na Denmark na Italia ikatoka sare pia na Finland katika kundi A.

Monday, July 15

Manchester United kumsajili Fabregas.

Klabu ya Manchester United imewasilisha ombi la kutaka kumsajili mcheza kiungo wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas.
Ripoti zinasema kuwa Manchester United inataka kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano.
Wasimamizi wa Barcelona kwa sasa wanajadili pendekezo hilo, lakini inaaminika kuwa kiasi walichopendekeza ni kidogo.
Licha ya kuwa Fabregas hajaomba kuruhusiwa kuondoka, lakini kuna fununu kuwa huenda akashawishika kurejea tena nchini England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, huenda akakubali kujiunga na Manchester United ikiwa wasimizi wa Barcelona watakubali kiasi kilichopendekezwa na Manchester United.


BBC.

Sunday, July 14

Rooney haendi kokote asema Moyes.


Kocha mpya wa Manchester United David Moyes, amekariri kuwa nyota wake Wayne Rooney atasalia na klabu hiyo na kamwe hana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anarejea nyumbani kutoka Thailand ambako timu hiyo imepiga kambi kambla ya kuanza kwa msimu, kutokana na jeraha la mguu.
Kumekuwa na fununu kuwa mchezaji huyo huenda akakihama klabu hiyo, licha ya Moyes kusisitiza kuwa Rooney hauzwi kwa lolote lile.
Klabu ya Chelsea, vile vile wako nchini Thailand na kocha wao mpya Jose Mourinho aliulizwa ikiwa ana nia ya kumsajili Rooney.
Lakini Mourinho alisema kwamba hana mazoea ya kuzungumza kuhusu wachezaji wa klabu nyingine lakini amekiri kuwa anampenda Rooney.
Kwa upande wake Moyes alisema kocha huyo wa Chelsea ana nia ya kumsajili mchezaji huyo ila hataki kusema wazi wazi.
Rooney, ambaye ameifunguia Manchester United magoli 197, baada ya kucheza mechi mia nne na mbili anatarajiwa kusalia nje ya uwanja wa muda wa wiki mbili zijazo kutokana na jeraha hilo na wala sio mwezi mmoja kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.

Thursday, July 11

Wanyama asajiliwa na Southampton.

Southampton imemsajili mcheza kiungo wa Celtic Victor Wanyama kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili na nusu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Cletic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, amesaini mkataba wa miaka minne na Southampton.
Wanyama, kutoka Kenya, aliteuliwa kuwa mchezaji bora mchanga katika ligi ya Scottland mwaka uliopita na alifunga bao wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona ambayo Celtic iliibuka na ushinda wa goli moja kwa bila.
Kiasi hicho ndicho cha juu zaidi kwa mchezaji yeyote kuuzwa nchini Scottland.
Wanyama vile vile amevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoma Kenya kushiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.
Kwingineko Swansea imekamilisha usajili wa Wilfreid Bonny kutoka kwa klabu ya Vitesse arnhem ya Uholanzi kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili kiwango ambacho ndicho kubwa zaidi kwa klabu hiyo kumnunua mchezaji yeyote.
Hata hivyo usajilki huo utategemea ikiwa mchezaji huyo atapewa kibali cha kufanya kazi nchini England.
Bonny ambaye alikuwa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya uholansi, alifunga magoli 21 baada ya kucheza mechi 30 msimu uliopita pekee.
Klabu ya Westham vile vile ilikuwa imewasilisha ombi la kutakakumsajili mchezaji huyo kutoka Ivory Coast lakini Swansea ikafanikiwa kwa kutoa kiasi cha juu.vic.

BBC.