Sunday, July 14

Rooney haendi kokote asema Moyes.


Kocha mpya wa Manchester United David Moyes, amekariri kuwa nyota wake Wayne Rooney atasalia na klabu hiyo na kamwe hana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, anarejea nyumbani kutoka Thailand ambako timu hiyo imepiga kambi kambla ya kuanza kwa msimu, kutokana na jeraha la mguu.
Kumekuwa na fununu kuwa mchezaji huyo huenda akakihama klabu hiyo, licha ya Moyes kusisitiza kuwa Rooney hauzwi kwa lolote lile.
Klabu ya Chelsea, vile vile wako nchini Thailand na kocha wao mpya Jose Mourinho aliulizwa ikiwa ana nia ya kumsajili Rooney.
Lakini Mourinho alisema kwamba hana mazoea ya kuzungumza kuhusu wachezaji wa klabu nyingine lakini amekiri kuwa anampenda Rooney.
Kwa upande wake Moyes alisema kocha huyo wa Chelsea ana nia ya kumsajili mchezaji huyo ila hataki kusema wazi wazi.
Rooney, ambaye ameifunguia Manchester United magoli 197, baada ya kucheza mechi mia nne na mbili anatarajiwa kusalia nje ya uwanja wa muda wa wiki mbili zijazo kutokana na jeraha hilo na wala sio mwezi mmoja kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.