Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

Tuesday, July 30

Uchaguzi utakuwa huru na haki asema Mugabe.


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametoa wito wa kuwepo amani katika uchaguzi mkuu ujao huku akiapa kuwa uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika siku ya JJumatano wiki hii, utakuwa wa huru na haki.
Pigeni kura kwa amani alisema Rais Mugabe alipokuwa anawahutubia wafuasi wake takriban 40,000 katika kampeni zake za mwisho zilizofanyika kwenye uwanja wa taifa wa michezo mjini Harare jana . Mugabe amesema bado mpaka sasa hakujashuhudiwa ghasia zozote katika siku za mwisho za kampeni ikilinganishwa na mwaka wa 2008.
Aliwaambia waandishi habari kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki kwa kuwa wapiga kura hawataelekezwa kupigia kura upande wowote, watachagua wenyewe ni nani atakayewaongoza tena.
Katika uchaguzi wa mwaka 2008 Tsvangirai alishinda katika maeneo mingi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi iliojawa na ghasia lakini baadaye akajiondoa katika duru ya pili baada ya takriban wanachama 200 wa upinzani kuuwawa.
Mwaka mmoja baada ya uchaguzi huo Tsvangirai na Mugabe wakaunda serikali ya muungano.
Raia wa Zimbabwe kupiga kura wiki hii
Sasa raia wa Zimbabwe siku ya Jumatano watamchagua rais wao pamoja na bunge jipya ikiwa ni miaka minne baada ya Mugabe aliyetawala nchi hiyo kwa miaka 34 kulazimika kugawana madaraka na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.
Hata hivyo Rais huyo aliye na umri wa miaja 89 ameonya dhidi ya mataifa ya kigeni kuingilia uchaguzi wa nchi yake akiangazia tawala zilizoangushwa baada ya maandamano nchini Misri na Libya. " Unaona kinachotokea Misri ni kwasababu walidanganywa ili wamuondoe rais wao, raia huko wanapigana huku mataifa ya Magharibi yakitazama tu ni kana kwamba hawajui walichokifanya katika nchi hiyo," Alisema Robert Mugabe.
Uhusiano kati ya Zimbabwe na mataifa ya Magharibi bado inabakia kuwa tete kufuatia vikwazo vya kimataifa ilivyoekewa nchi hiyo tangu mwaka wa 2002.
Kando na Mugabe kuwa katika kinyan'ganyiro cha kuwania muhula mwengine, amewaambia waandishi habari kwamba hata mwaka wa 2018 atakuwa katika mbio hizo hizo za kutaka kuiongoza nchi hiyo.
Morgan Tsvangirai afanya kampeni za mwisho
Kwa upande wake Waziri mkuu Morgan Tsvangirai anafanya kampeni zake za mwisho katika ukumbi mkubwa ulioko karibu na makao makuu ya chama cha ZANU-PF siku mbili kabla ya kufanyika uchaguzi huo mkuu. Wakati huo huo afisa mkuu wa chama cha MDC cha waziri mkuu, alikamatwa jana kwa madai ya kuripoti wizi wa kura katika kura za mwazo zilizopigwa nchini humo ambazo ni za maafisa wa polisi na jeshi.
Chama hicho kimesema Morgan Komichi alikamatwa baada ya kuripoti kwa tume ya uchaguzi kuwa karatasi za kupigia kura zilizokuwa na kura za chama hicho zilitupwa.
Polisi nchini humo sasa wametishia kumfungulia mashtaka Komichi kwa kuingilia sheria za tume ya uchaguzi iwapo hatasema ni nani aliyempa taarifa hizo za kutupwa kwa karatasi hizo za kupigia kura, zuilizokuwa na kura za MDC.

Tuesday, July 9

Brotherhood yapinga ratiba ya uchaguzi Misri


Maafisa wakuu wa chama cha Muslim Brotherhood, wamepinga vikali pendekezo la rais wa mpito Adly Mansour kuweka ratiba ya kuandaa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Mmoja wa viongozi wa chama hicho, Essam al-Erian anasema kuwa mpango huo utakaojumuisha mabadiliko ya kikatiba na kura mwaka ujao unarejesha nchi hiyo ilipokuwa baada ya mapinduzi ya kumwondoa mamlakani Hosni Mubarak.
Rais wa mpito alitangaza kuwa uchaguzi utafanyika mwaka ujao katika juhudi zake za kutuliza maandamano na hali ya taharuki nchini humo.
Tangazo hilo lilitolewa wakati mgogoro ukizidi kati ya jeshi na wafuasi wa rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi karibu na kambi ya jeshi mjini Cairo ambako zaidi ya watu 50 waliuawa hapo jana wakati wa mapigano na wanajeshi.
Aidha tangazo la Rais Adly Mansour, linaashiria mageuzi katika katiba kwa kuitisha kura ya maoni ambayo huenda ikachangia kufanyika kwa uchaguzi mwaka ujao.
Hii inakuja wakati ambapo watu 51 wamethibitishwa kuuawa mjini Cairo.
Chama cha Muslim Brotherhood kinasema kuwa wanachama wake walipigwa risasi wakati walipokuwa wanakesha nje ya makano ambapo Morsi anazuiliwa, lakini jeshi linasema liliwafyatulia risasi kwani waandamanaji nao walikuwa wamejihami.
Rais Morsi, aliyekuwa rais wa kiisilamu na wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, aliondolewa mamlakani na jeshi wiki jana baada ya maandamano makubwa ya kumpinga kufanyika.
Wafuasi wake wanatuhumu jeshi kwa kufanya mapinduzi, lakini wapinzani wake wanasema hatua hiyo ni mwendelezo wa mapinduzi yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak mwaka 2011.

Bwana Mansour alitoa amri hiyo Jumatatu jioni.

Amri hiyo inasema kuwa jopo la kufanyia katiba marekebisho ambalo lilifutwa kazi wiki jana, litaundwa tena katika kipindi cha siku 15.
Mabadiliko hayo kisha yatapigiwa kura ya maoni. Mchakato utapangwa kufanyika katika muda wa miezi minne.
Baada ya kura ya maoni , uchaguzi wa wabunge huenda ukafanyika mapema mwaka 2014.
Hatimaye uchaguzi utafanyika punde baada ya bunge jipya kuundwa.



Sunday, July 7

Mansour ajaribu kuweka udhibiti wake Misri


Rais mpya wa Misri ameanza kuimarisha madaraka yake na udhibiti wa mitaa hata wakati wapinzani wake wa chama cha Kiislamu wamesema kuwa mamlaka yake ni kinyume na sheria na wakidai rais Mursi arejeshwe madarakani.
Kuondolewa kwa Morsi madarakani kwa njia ya mapinduzi kumesababisha maandamano makubwa pamoja na mapambano ya mitaani kati ya makundi hasimu.
ELBaradei hatakiwi
Kuonesha hali ya mgawanyiko mkubwa unaomkabili kiongozi huyo asiye na uzoefu wa kutosha , Adly Mansour, ofisi yake imesema kuwa kiongozi anayependelea mageuzi Mohammed ElBaradei ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa mpito lakini kauli hiyo ilibadilishwa haraka baadaye na kusema kuwa mashauriano bado yanaendelea .
Mwanasiasa ambaye yuko karibu na ElBaradei amesema hatua hiyo ya kubadilisha uamuzi inatokana na upinzani kutoka kwa chama cha kihafidhina kinachofuata siasa kali zinazoegemea dini ya Kiislamu ambacho utawala mpya unataka kushirikiana nacho.
Utawala wa Mansour , wakati huo huo , umeanza kujaribu kuondoa kile Morsi alichokijenga. Amemuondoa mkuu wa usalama wa taifa na mnadhimu mkuu wa ikulu ya nchi hiyo.
Viongozi wabaki korokoroni
Waendesha mashtaka, wakati huo huo , wameamuru viongozi wakuu wa chama cha Morsi cha udugu wa Kiislamu ambao wamewekwa kizuizini washikiliwe kwa muda wa siku 15 wakisubiri uchunguzi uendelee kuhusiana na kushambuliwa na kuuwawa kwa waandamanaji wanane wiki iliyopita.
Hakuna ghasia kubwa zilizoripotiwa kati ya waungaji mkono na wapinzani wa Morsi wakati pande hizo mbili zimejikusanya tena baada ya usiku wa mapambano makali ambayo yameufanya mji wa Cairo kuwa eneo la mapambano. Mapigano pia yamekuwa makali katika mji wa bandari wa Alexandria, ambako maelfu ya wafuasia wa kila upande walipigana kwa risasi, mabomu ya moto na virungu.
Ghasia za Ijumaa zimesababisha watu 36 kuuwawa, na kufikisha idadi ya karibu watu 75 waliouwawa tangu ghasia hizo kuzuka hapo Juni 30, wakati mamilioni ya waandamanaji wakiingia mitaani katika mkesha wa mwaka wa kwanza tangu Morsi kuingia madarakani kidemokrasia.
Morsi ambaye ni mhandisi aliyepata mafunzo yake nchini Marekani ambaye anashutumiwa sana na wakosoaji kwa kuhodhi madaraka binafsi na kwa ajili ya chama chake cha udugu wa Kiislamu pamoja na kushindwa kwake kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia ya kiuchumi , ameendelea kubaki kizuwizini katika eneo ambalo halijilikani. 
Wasi wasi wazidi
Hali ya wasiwasi imeendelea kuongezeka wakati mamia kwa maelfu ya wafuasia wa Morsi wakiingia mitaani kwa siku ya tatu karibu na msikiti katika eneo la mji wa Cairo ambalo kwa kawaida ni ngome kuu ya chama chake, wakiimba kauli mbiu za hasira dhidi ya kile wanachokiita mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na jenerali wa jeshi Abdel-Fattah el-Sissi. Jenerali huyo wa jeshi amekana kuwa amefanya mapinduzi ya jeshi, akisema kuwa alikuwa anachukua hatua za matakwa ya mamilioni ya Wamisri wanaoandamana dhidi ya rais huyo wa zamani.

Thursday, July 4

Jeshi la Misri lampindua Mursi.


Maelfu ya Wamisri wanasherehekea kupinduliwa Rais Mohammed Mursi, huku kukiwa na taarifa kwamba jeshi limeanza kuwakamata viongozi wa juu wa Udugu wa Kiislamu na wasiwasi ikiwa hatua hii italeta muafaka wa kisiasa.
Kwa siku nzima ya jana (04 Julai), watu walikuwa wakisubiri kwa hamu muda wa mwisho aliopewa Raus Mursi na jeshi, na jioni yake maelfu ya wapinzani wa kiongozi huyo wa mwanzo kuchaguliwa kidemokrasia walizidi kumiminika kwenye viwanja vya Tahrir na kasri ya rais. Hali ilikuwa ya amani zaidi kuliko ilivyokuwa katika siku za hivi karibuni.
Pale waziri wa ulinzi alipoanza kutoa hotuba yake iliyongojewa kwa hamu na kwa muda mrefu, umma ulipiga kelele za “Amani!Amani!”, lakini dakika chache baadaye umma huo ukaripuka kwa vifijo na nderemo na uwanja wa Tahriri ukageuka mara moja kuwa uwanja wa tamasha. Fashifashi zikalitanda anga, na watu wakavaana miilini huku wakifuta machozi ya furaha. Sharif, profesa wa chuo kikuu ni mmoja wao.
“Nina furaha ya kunichania nguo hapa, kuona kwamba Wamisri wa kila tabaka wapo uwanjani. Mtu anaweza kusema kwamba huku ni kuachiliwa uhuru wetu kutoka gerezani mwa wenye siasa kali. Udugu wa Kiislamu wamesababisha matatizo mengi sana.” Amesema Sharif.
Sharif alisisitiza kwamba wote ni Wamisri na sio Waislamu au Wakristo, kwamba kwa miaka 7000 wamekuwa wakinywa maji mamoja na wakivuta hewa moja. Kando ya Sharif, mtu mwengine alijiangusha chini na kusujudu kumshukuru Mungu, huku macho yake yamerowa machozi.
Bado kungali na maswali kadhaa.
Lakini kando ya furaha hizi kubwa, watu hawa waliopeperusha bendera kulipongeza jeshi kwa kumuondoa Mursi, bado wana maswali kadhaa ya kujijibu. Jeshi, upinzani, wawakilishi wa Kanisa la Koptik na wa dini ya Kiislamu, walisema wamekubaliana kwamba Mkuu wa Mahakama ya Kikatiba awe rais wa kipindi cha mpito, lakini utaratibu mzima kuelekea uchaguzi mpya bado hauko wazi.
Pia haifahamiki hatima ya Rais Mursi na wenzake wa kundi la Udugu wa Kiislamu, ambao taarifa zinasema wanashikiliwa na jeshi. Baadhi ya walio Uwanja wa Tahriri, kama Nadir, wanapajua wanapotaka Mursi awepo kwa sasa.
“Lazima awe yuko gerezani na lazima mumshitaki. Watu wengi wameuawa wakati wa uongozi wake na hatuwezi kuwasahau.” Anasema Nadir.
Lakini Mursi alikuwa rais wa kwanza kuingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasia, akishinda zaidi ya asilimia 50 ya kura, na hivyo uhalali na nguvu zake haziwezi kupuuziwa kisiasa na hata kisheria.
Bado haifahamiki ikiwa wafuasi wa Udugu wa Kiislamu, ambao waliripuka kwa ghadhabu wakati mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi, alipokuwa akitangaza mapinduzi yake usiku wa jana, watajiunga na kipindi cha mpito, ama nao wataendelea kuandamana na hivyo kuikwamisha tena nchi kisiasa.
Kwa vyovyote vile, bado mambo hayajesha kwenye taifa hilo kongwe kaskazini mwa Afrika.

Wednesday, July 3

Obama ahitimisha ziara ya Afrika


Rais wa Marekani Barack Obama amehitimisha ziara yake barani Afrika nchini Tanzania huku akikutana na mtangulizi wake George W. Bush katika kumbukumbu ya wahanga wa mashambulizi ya ugaidi mwaka 1998 mjini Dar es Salaam.
Rais Obama na familia yake walikuwa jijini Dar es Salaam katika siku ya mwisho ya ziara iliyodumu wiki nzima, wakati Bush na mkewe Laura wapo jijini humo kama wenyeji wa mkutano kuhusu nafasi ya wake wa marais katika kuleta mabadiliko nchini mwao. Bush aliungana na rais Obama katika hafla ya kuweka maua kuwakumbuka wahanga wa Kitanzania wa mashambulizi yaliyotokea wakati mmoja dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwezi Agosti 1998, ambayo yanadaiwa kupangwa na Osama bin Laden.Marais hao wawili waliinamisha vichwa vyao wakati mwanajeshi wa majini akiweka maua ya rangi nyekundu, nyeupe na bluu katika kumbukumbu hiyo. Baada ya dakika chache, wawili hao walishikana mikono na manusura wa mashambulizi hayo pamoja na jamaa za waliouawa kabla ya kurejea tena ubalozini baada ya dakika chache tu.
Wake zao nao washiriki mjadala
Wakati huo, wake zao walikuwa wakishiriki katika mjadala wa umma uliokuwa ukiendeshwa na mwandishi wa habari wa Kimarekani Cokie Roberts. Mke wa Obama alisema alitaka kuonekana na Laura Bush kwa sababu "nampenda mwanamke huyo." "Ni kama klabu fulani ya wanafunzi wa chuo kikuu nadhani," alijibu Laura Bush kimaskhara. Lengo lao lilikuwa kuwahimiza wake wa marais wa Afrika, ambao wengi wao walikuwepo katika hadhira, kupandisha sauti zao kwa ajili ya mambo walio na mapenzi nayo.
Wakati watu wakichambua viatu vyetu na kushughulikia nywele zetu--" alianza mke wa Obama. " Hata tukiwa na mabango," aliingilia kati Laura Bush na kusababisha kicheko. Michelle alionyesha kustajabishwa kuwa mfumo wa nyewele zake unavutia waandishi wengi wa habari. "Nani angefikiria hivyo?" Laura alisema anampa pole Michelle kwa sababu hata nyewele za binti yake Barbara zilisababisha msukosuko wakati fulani.
Lakini Michelle Obama alisema mwishowe watu wanaancha kuangalia mabango yao na kuanza kuangalia kile walichosimama mbele yake. Akiwa barani Afrika, Obama amemsifu Bush mara kwa mara kwa kusaidia kuokoa mamilioni ya maisha kwa kufadhili matibabu ya ugonjwa wa ukimwi. "Napenda kumshukuru tena nikiwa katika ardhi ya Afrika kwa niaba ya watu wa Marekani, kwa kuonyesha jinsi ukarimu wa wamarekani na muono wa mbali vinavyoweza kubadilisha maisha ya watu," alisema Obama siku ya Jumatatu.Washirika badala ya wafadhili
Lakini rais huyo alisema pia anataka kubadilisha mkakati wa Marekani kwa Afrika. "Tunatafakkari kuwa na ruwaza mpya ambayo msingi wake si tu msaada, bali pia ushirikiano wa kibiashara," alisema. "Mwisho wa siku, lengo hapa ni kwa Afrika kuijenga Afrika kwa ajili ya Waafrika," Obama alisema na kuongeza kuwa kazi yao kama Wamarekani ni kuwa washirika katika mchakato huo.
Katika moyo huo, Obama alitangaza mkataba mpya wa kibiashara na mataifa ya kanda ya mashariki mwa Afrika, na programu ya kuongeza upatikanaji wa umeme kwa Waafrika wasiokuwa na nishati hiyo. Ugunduzi mmoja unaoweza kusaidia katika suala la umeme ni "Soccket ball," ambao ni mpira uliyogunduliwa na wasomi wawili wa chuo kikuu cha Harvard. Mpira huo una mtambo ndani yake unaofanana na penduli, ambao unafua nishati mwendo wakati unachezwa na kuihifadhi. Watengenezaji wake wanasema ukichezwa kwa dakika 30 unaweza kuwasha taa ya LED kwa masaa matatu. Mpango ni kuisambaza mipira hiyo kwa watoto barani Afrika.Programu ya Power Africa
Wakati wa ziara yake katika mtambo wa umeme wa Ubungo na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, Obama aliupiga mpira huo, na kusema kuwa mipira hiyo itaanza kusambazwa kote barani Afrika. Mtambo huo wa Ubungo ulidhaminiwa kwa mkopo usio na riba kutoka Marekani na kujengwa na kampuni ya Marekani ya American Corpration General Electric and Symbion.
Katika hotuba yake baada ya ziara hiyo, Obama aliipigia debe programu ya umeme ya 'Power Africa' akiita kuwa ni ushindi kwa makampuni ya Afrika na ya Marekani. Pia alizungumzia ziara yake ya wiki nzima, na kukumbuka baadhi ya watu aliokutana nao njiani, akiwemo mkulima mmoja wa kike nchini Senegal na vijana mjini Soweto. "Nimetiwa moyo kwa sababu nimeshawishika kuwa ikiwa njia sahihi zitafuatwa, Afrika na watu wake wanaweza kuanzisha enzi mpya ya mafanikio," alisema Obama.

Tuesday, July 2

Serikali yapinga onyo la jeshi Misri


Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Misri Mohammed Morsi imesema kuwa rais huyo atashikilia mpango wake wa kuleta maridhiano ya kitaifa ili kutatua mzozo wa kisiasa unaokabili taifa hilo.
Hilo ndilo tamko la kwanza kutoka kwa rais huyo tangu jeshi litoe makataa ya saa arobaini na nane kuwataka wanasiasa kutoka pande zote kutatua mgogoro huo.
Taarifa hiyo ya rais imesema kuwa hatua hiyo ya jeshi kuingilia kati itazua hali ya suitofahamu zaidi.
Jeshi limetoa makataa ya saa arobaini na nane kwa Morsi kutatua mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo la sivyo watachukua hatua.
Jeshi limekanusha madai kuwa makataa hayo ni sawa mapinduzi ya kijeshi.
Serikali imesema kuwa Morsi amewasiliana na rais Barack Obama kuhusu hali ya kisiasa inayoshuhudiwa Misri.
Wakati huohuo, shirika la habari la kitaifa Misri, limeripoti kuwa waziri wa mambo ya nje Mohamed Kamel Amr amejiuzulu.
Ikiwa ombi lake litakubaliwa, atakuwa mmoja wa mawaziri wengine watatno ambao wamejiuzulu kufuatia mgogoro huo wa kisiasa.
Mnamo jumapili, mamilioni walifanya maandamano wakimtaka rais ajiuzulu.
Maandamano mengine makubwa yalishuhudiwa Jumatu huku ripoti zikisema kuwa watu wanane waliuawa wakati waandamananaji walipovamia makao makuu ya chama tawala cha Muslim Brotherhood.
Wapinzani wa Morsi,wanamkosoa kwa kuweka maslahi ya chama mbele huku akiwapuuza wale wasiounga chama hicho.
Morsi alichaguliwa kama rais wa kwanza wa kiisilamu katika uchaguzi wa mwezi Juni mwaka 2012 tarehe 30 bbaada ya kushinda uchaguzi uliotazamiwa na wengi kuwa huru na wa haki baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak.

Thursday, June 20

Obama aacha gumzo Berlin

Akikumbushia historia kali ya mji wa Berlin uliyogawika wakati mmoja, rais Barack Obama amezitahadharisha Marekani na Ulaya dhidi ya kuridhika kunakosababishwa na amani, huku akiapa kupunguza silaha za nyuklia.
Rais Obama pia alitangaza kuwa programu yake ya udukuzi wa mawasiliano iliyozua zogo duniani, imenusuru maisha katika pande zote za Atlantiki. Akihutubia umati uliokusanyika katika lango kuu la Brandenburg, Obama alisema ipo haja ya kupunguza kwa sana tu, silaha za nyuklia za Marekani na Urusi, ili kuondoka katika hali ya kivita inayoendelea kuchochea kutoaminiana baina ya serikali za mataifa hayo.
"Tunaweza tusiishi katika hofu ya maangamizi ya nyuklia, lakini maadam silaha za nyuklia bado zinaendelea kuwepo, hatuna usalama wa kweli," alisema Obama wakati akihitimisha ziara ya siku tatu barani Ulaya, ambayo ndiyo ya kwanza tangu aliposhinda muhula wa pili.
Jinamizi la udukuzi wa mawasiliano lamfuata Berlin
Obama anakabiliwa na migogoro ya ndani pamoja na changamoto za sera ya kigeni, ambavyo vinamvurugia malengo yake ya muhula wa pili. Masuala mawili - vita vikali vinavyoendelea nchini Syria, na program ya udukuzi wa mawasiliano - vilimzonga Obama wakati wa ziara yake nchini Ujerumani, na vile vile katika mkutano wa kundi la mataifa nane yalioendelea kiviwanda, G8 mjini Belfast, Ireland ya Kaskazini mapema wiki hii.
Ujerumani, nchi inayolinda sana faragha, ilitaka hasa majibu kutoka kwa Obama kuhusiana na Programu hiyo inayoendeshwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA. Kansela Angela Merkel, alitumia mkutano wake na Obama kwa waandishi wa habari, kutaka kuwepo na uangalifu, katika kutathmini wasiwasi kuhusu faragha, inagwa aliepuka kukwaruzana hadharani na rais.
"Kunahitajika kuwepo uwiano, haya ni mapambano ambayo yataendelea," alisema Merkel. Obama alitoa utetezi mrefu wa programu hiyo iliyoidhinishwa na mahakama, akiielezea kama juhudi makhsusi ambayo imesaidia kunusuru maisha. "Tunafahamu kuhusu mashambulizi yasiyopungua 50 ya kigaidi yaliyozuiwa kwa kutumia taarifa hizi, si tu nchini Marekani, bali pia katika maeneo mengine kama hapa Ujerumani."
Tukio kuu la ziara ya Obama lilikuwa hotuba ya mchana katika lango la Brandenburg, ambako kulikuwa na ukuta wa Berlin uliyougawa mji huo kati ya mashariki na magharibi. Obama, aliesimama nyuma ya kidirisha cha bilauri isiyopita risasi, alizungumza kutoka upande wa mashariki wa lango hilo, eneo ambalo enzi hizo haikuwa rahisi kwa rais wa Marekani kukanyaga.
Alinganishwa na Kennedy
Hotuba ya raia Obama ililinganishwa na ile maarufu ya John F. Kennedy ya "Ich bin ein Berliner" (Mimi ni mkaazi wa Berlin), aliyoitoa miaka 50 iliyopita, na vile vile mapokezi ya kihitoria aliyoyapata Obama mwenyewe alipowasili mjini humo akiwa mgombea wa urais mwaka 2008. Zaidi ya watu 200,000 walifurika katika eneo la karibu na uwanja huo kusikiliza hotuba hiyo, iliyoakisi matarajio makubwa waliokuwa nayo raia wa Ulaya kwa mwanasiasa chipukizi wa Marekani.
Wakati huu akiwa katika mwaka wake wa tano kama rais, Obama bado anaendelea maarufu barani Ulaya. Lakini umati uliokusanyika kumsikiliza siku ya Jumatano ulikuwa mdogo sana ikilinganishwa na mwaka 2008. Hotuba yake iligusia masuala kadhaa yanayotoa changamoto kwa dunia, ambapo alitoa wito kwa mataifa ya magharibi kuwasha upya mzuka uliyoonyesha na Berlin wakati ambapo raia wengi walikuwa wakipambana kuunganisha tena mji huo wakati wa vita baridi.
"Vitisho vya sasa siyo kama ilivyokuwa nusu karne iliyopita, lakini mapambano yanaendelea," alisema. "Na nimekuja hapa katika mji huu wa matumaini kwa sababu mitihani ya wakati wetu inatutaka tuwe na roho ya kupambana ambayo mji wa Berlin ulikuwa nayo nusu karne iliyopita."
Mkutano wa nyuklia mwaka 2016
Obama alisema Marekani inaandaa mkutano mwaka 2016, kuhusu juhudi za usalama wa silaha za nyuklia zisizo hifadhiwa vizuri duniani kote, na kuongeza kuwa utawala wake utajitahidi kutafuta uungwaji mkono nchini Marekani, kuridhia Mkataba wa unaopiga marufuku majaribio ya silaha za nyuklia.
Umati wa wageni waalikwa karibu 6000 walivumilia jua kali kushangilia mapendekezo ya Obama kuhusu silaha za nyuklia, na dhamira yake ya kuongeza mara mbili, juhudi za kufunga gereza la Guantanamo lililoko nchini Cuba.
Obama aliondoka mjini Berlin kwa ndege yake ya Air Force One majira ya saa nne usiku, na kuhitimisha ziara iliyodumu kwa masaa 25, katika jiji ambalo wakati mmoja lilikuwa mahali pa hatari kati ya muungano wa kisovieti na mataifa ya magharibi, na ambako vita baridi vilitisha mara nyingi kuripuka katika vita vingine vya dunia. Utawala wa Kikomunisti wa Ujerumani Mashariki ulijenga ukuta wa Berlin, ambao uliugawa mji huo kati ya mashariki na magharibi mwaka 1961.
Lango la Brandenburg, ambako Obama alitoa hotuba yake, ni jengo la tao lenye njia tano, ambalo wakati mmoja lilisimama karibu na ukuta wa Berlin. Ukuta huo ulifunguliwa Novemba mwaka 1989, na ulivunjwa katika miezi iliyofuata, na Ujerumani iliungana tena mwaka 1990.
Mwaka 1994 rais Bill Clinton alikuwa wa kwanza kutoa hotuba kwa Berlin iliyoungana, na kama Obama, yeye pia alizungumza katika uwanja wa Pariser, katika upande wa mashariki wa lango hilo, akiahidi kuwa ubalozi mpya wa Marekani ungejengwa katika upande wa pili. Ubalozi huo ulinfunguliwa mwaka 2008.

DW.

Thursday, February 14

Vigogo wa uraisi CCM 2015


UCHAGUZI wa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanywa na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho Jumatatu wiki hii mjini Dodoma, ni kama unabadili mwelekeo wa siasa za ndani za chama hicho kikongwe nchini.
Tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani miaka saba iliyopita na kupewa kofia ya uenyekiti wa CCM, chama hicho kimekuwa kwenye minyukano ya siasa za visasi kiasi kwamba hakijawahi kuwa na utulivu wa kisiasa kama ilivyo sasa, miezi michache baada ya kufanyika mabadiliko kadhaa ya kiuongozi.
Uteuzi na baadaye uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu umeweka kando baadhi ya vigogo wa kisiasa hasa waliokuwa wakitajwa katika harakati za kuusaka urais katika uchaguzi wa 2015 na kuziingiza sura mpya ambazo huenda baadhi yao wanaweza kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Ushirikiano wa

Wednesday, January 23

CHADEMA yawashukia Nape, Mwigulu


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.

Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa
Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.

Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo