Mchezaji soka Mnigeria Shola Ameobi amesema kuwa ana
furaha isiyo na kifani kwa kuingiza bao lake la kwanza katika mechi ya
kitaifa na ya kirafiki kati ya Nigeria na Burkina Faso ambapo Nigeria
ilishinda kwa mabao 4-1 .
Mchezaji huyo anayechezea Newcastle aliambia BBC kuwa , hatimaye ameingiza bao na kuwa ana furaha sana .Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya kitaifa ya vijana Uingereza, alikubaliwa tu mwaka jana Novemba kuchezea Super Eagles, na hadi kufikia sasa, amecheza mara nne, anatumai kuwa kuanzia sasa ataweza kuwa kiungo muhimu kwa timu ya taifa Nigeria ambao ni mabingwa wa afrika.
Wakati huohuo, Nigeria ilimaliza ya kwanza katika kundi F kwenye michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa nchi za Afrika, kutokana na ushindi wao dhidi ya Mali ambapo walishinda kwa mabao mawili bila mwishoni mwa wiki.
Sasa wanasubiri draw ya Jumatatu kwa michuano wa mwisho ambayo itawahusisha washindi kumi wa mechi zilizopita.
Haya ndiyo matokeo ya mechi za kirafiki zilizochezwa Jumanne zikihusisha timu za Afrika.
Chanzo: bbc