Mvua kubwa mno katika wiki za hivi karibuni zimesababisha mto Shabelle kuvunja kingo zake kwenye mikoa ya Somalia ya Hiran, Shabelle ya Kati na Shabelle ya Chini, ikiwaacha mamia ya familia kukosa makazi na kuhitaji sana usaidizi kutoka wakala wa misaada wa kitaifa na kimataifa kusaidia.Gavana wa Hiran Abdi Farah Laqanyo alisema mwitikio wa ukoaji wa taratibu kwenye mafuriko umechanganya utawala wake, na kutuhumu asasi za kitaifa na kimataifa kwa kupuuza hali ya hatari ya kibinadamu inayokabili mamia ya familia ambazo zilikimbilia maeneo ya karibu na Beledweyne.
"Ninatoa wito kwa [mashirika] kuchukua hatua katika hali ya kibinadamu kusaidia wale walioathiriwa vibaya na kukosa makazi, kwa sababu mvua na mito iliyofurika imeingilia harakati za watu katika maeneo ya makazi ya jiji hilo, ambalo limezungukwa na nyanda zenye miamba," aliiambia Sabahi.
"Wenyeji pia wanapata ugumu kwenda kununua vitu, kwani maji yanasomba lundo la matope, uchafu na mwamba kwenye makazi na kwenye mitaa yaliyoharibika, hali inayosababisha kuenea kwa hali kama vile kipindupindu mbaya, malaria na utapiamlo," alisema.
Mabwawa mengi kandokando ya Mto Shabelle yalishindwa au kuharibika kisasi cha kushindwa kutengenezwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza mwaka 1991, gavana huyo alisema. Mafuriko yameharibu maisha ya wananchi na kuharibu mazao, nyumba na majengo madogomadogo, wakati magonjwa ya kuambukiza, utapia mlo na umaskini imewakumba wanakijiji.
Gavana wa Shabelle ya Chini Abdiqadir Mohamed Nur alisema mvua na mafuriko zimeharibu makazi kadhaa huko Janaale na Wanlaweyn, na kuharibu mali na kuwafanya wamiliki kuhama pasipo kutarajia. Wakaazi wamekimbilia kwenye manispaa na mashirika ya misaada kwa ajili ya kusaidia na huduma za afya, kwani maji machafu yanayotoka majumbani yamechanganyikana na maji ya mafuriko na kusababisha mgogoro wa afya ya umma, alisema.
Mafuriko ya Mto Shabelle yamefanya mji wa Beledweyne kutoendelea na chochote na kusomba dazeni za vijiji, migomba na mashamba ya nafaka. Watoto wanne wamekufa mjini hapo, alisema.
"Tumeorodhesha ajali za barabarani na kuanguka kwa majengo mengi kwani mafuriko yamewatisha wakaazi ambao wamekuwa wakiagiza makazi bora mara kadhaa kabla ya msiba wa msimu huu kwa sababu walijua majengo machakavu hayatahimili," Nur aliiambia Sabahi.
Miji yageuka kuwa vinamasi
Deqa Nurani Said, mama mwenye watoto nane mwenye umri wa miaka 32 huko Wanlaweyn, alisema alijihifadhi katika shule ya msingi ya umma, lakini mamia ya wakaazi wengine walikuwa wakilala katika eneo la wazi, karibu na barabara kuu. Hakuna shirika lililowapa msaada na huduma za uokozi au msaada wa matibabu, au kujaribu kusaidia familia zilizoathirika,alisema.
"Tunakabiliwa na hatari ya njaa na magonjwa na joto viko chini sana," aliiambia Sabahi. "Mvua imeendelea kunyesha sana katika wiki chache zilizopita. Mamia ya wakaazi wamelazimishwa kuhama nyumba zao, kwani mafuriko yamesomba nyumba zote na maghala mjini, ambako hakuna miinuko yoyote ya kuwaokoa dhidi ya maji ya mafuriko yanayosambaa. Hatujaona pia operesheni yoyote ya kutoa maji au ujenzi mpya wa kingo za mito"
Gavana wa Shabelle ya Kati Abdi Jinow Alasow alisema mafuriko yamewalazimisha wakaazi huko Jowhar kukimbia usiku baada ya maji kusomba vibanda vyao. Mafuriko pia yamekata barabara, njia za simu na umeme, kuwatenganisha wakaazi katika vitongoji vyao.
Alasow alisema mamia ya familia zinaishi mitaani. Maisha huko Jowhar yamesimama katika sekta nyingi muhimu, alisema, maji taka yamefurika kwa sababu hakuna njia za maji taka.
"Mji wa Jowhar, ambao unajulikana sana kwa kilimo cha mpunga na mbogamboga, umekuwa na usiku wa kusikitisha kutokana na mvua kubwa, ambazo zimesomba mto," aliiambia Sabahi. "Jiji halijawahi kuona mvua nyingi kama hiyo. Saa nane za mafuriko zilitosha kubomoa mitaa yote ya mji mkongwe, kugeuza baadhi kuwa vinamasi."
SABAHI ONLINE.