Bingwa wa dunia wa Tenis kwa wanawake, Serena
Williams ameshinda kwa mara ya kumi na saba shindano la US Open, katika
fainali lliyokuwa yenye mbwembwe dhidi ya Victoria Azarenka katika
uwanja wa Flushing Meadows.
Lakini baada ya ushindani mkali kutoka kwa Azarenka, Williams alilazimika kujitahidi zaidi ya alivyokuwa anacheza ili aweweze kupata ushindi kama ilivyokuwa katika michezo mingine 16 iliyopita ambapo aliweza kushinda.
Azarenka, mwenye umri wa miaka 24, aliwahi kumshinda Williams mara mbili mwaka huu , mara ya mwisho kwenye mchezo uliochezwa wa kirafiki eneo la Cincinnati mkesha wa shindano la US Open, mwaka huu na kujiamini kuwa angeweza kumshinda mmarekani kwenye ukumbi mkubwa.
Williams alionekana kuwa katika hali nzuri wakati wa shindano lote.
Chanzo: bbc