Saturday, January 26

Drogba akiri ni vigumu kutwaa ubingwa AFCON

NAHODHA Ivory Coast, Didier Drogba amesema timu yake itakuwa na wakati mgumu kutwaa kombe la Afrika msimu huu baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Togo katika mchezo wao wa kwanza.
Ni kweli tunataka kushinda, lakini kuna timu nyingine 15 nazo zinataka ubingwa huu, alisema Drogba.
Itakuwa ni ngumu kwetu kuchukua ubingwa huu, lakini tutahakikisha tunapambana hadi dakika ya mwisho.

Kwa mara ya

tano mfululizo Ivory Coast ndiyo timu inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini mwisho wanaondoka mikono mitupu. Watu wanataka sisi tuchukue ubingwa, lakini si rahisi kama hivyo, alisema Drogba. Hata hivyo huo ndiyo mpira.

Drogba alisema Ivory Coast,

inaongoza kwa ubora Afrika, lakini huwezi kuzibeza timu nyingine kutoka Afrika Magharibi.
Hata hivyo, nahodha huyo wa Ivory Coast, anaamini wakipata ubingwa utasaidia kurudisha umoja wa nchi yao.
Ubingwa utakuwa na maana kubwa kwa Ivory Coast kwa sababu timu hii imekuwa kwa pamoja kwa zaidi ya miaka10 sasa. Tumekuwa na kujifunza mengi kama wachezaji, alisema Drogba.
Nafikiri utakuwa wakati mwafaka tukitwaa ubingwa kwa ajili ya nchi yetu. Tunachopaswa kufanya ni kusahau yaliyopita na kujipanga kwa lengo la kurudisha umoja wa nchi yetu.

Ivory Coast itacheza na Algeria kesho kabla ya kuivaa Tunisia kwenye mchezo wa mwisho wa kundi lao.