![]() |
Mtu pesa bwana asikudanganye mtu. |
Mbali na kushikiliwa kwa polisi huyo, ofisa mwenye
cheo cha Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), amesimamishwa
kazi kwa madai ya kuhusika na mtandao huo wa utapeli.
Imebainika kuwa ofisa huyo alitapeli vijana 154 wa
kidato cha nne na sita kuwa angewawezesha kujiunga na Jeshi la Polisi
hivyo kujikusanyia Sh700,000 na
Sh900,000.
Sh900,000.
Habari za uhakika kutoka makao makuu ya polisi
jijini, zimeeleza koplo huyo aliamriwa na wakuu wake wa kazi kwenda
kujisalimisha mwenyewe Chuo cha polisi Moshi zamani kikijulikana kama
CCP.
“Tarehe 6.2.2013 ndiyo aliripoti kwa mkuu wa chuo
kule Moshi na kuwekwa mahabusu akisubiri kufunguliwa mashtaka ya
kijeshi,”amedokeza Ofisa mmoja makao makuu ya polisi Dar.
Habari hizo zimedai Oktoba 13,2012, Ofisa huyo wa
Polisi alighushi saini ya Ofisa wa Utawala makao makuu ya polisi,
Thobias Andengenye na kutuma simu ya upepo CCP ikiwa na majina ya vijana
hao.
Simu hiyo iliyotumwa kwa Commandant Moshi Police
Academy ikimwagiza mkuu wa chuo hicho cha Polisi awapokee vijana hao 154
kwa kuwa usajili wao umekamilika hivyo waingie chuoni.
Simu hiyo ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona,
inaendelea kusomeka kuwa” Wapokee ili waungane na wenzao kwa usajili wa
chuo ili waendelee na mafunzo ya awali ya askari polisi”.
Taarifa zaidi zinadai kuwa simu hiyo iliyokuwa na
sahihi ya T.B. Andengenye (SACP), haikutumwa moja kwa moja CCP bali
ilipitia Polisi Moshi na kupelekwa kwa mkono chuoni.
Baada ya siri kifichuka, Polisi makao makuu Dar es
Salaam walimwita koplo huyo na kumuamuru aende mwenyewe CCP Moshi
ambako aliripoti juzi na kuwekwa mahabusu.
Juhudi za kumpata Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Advera Senso ili kufafanua juu ya suala hilo ziligonga mwamba baada ya
simu yake kuita bila kupokelewa.