Matokeo ya mwanzoya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta akiwa anaongoza kwa asilimia hamsini na nne dhidi ya Raila Odinga aliye na asilimia arobaini na moja.
Ni uchaguzi ambao mamilioni ya wakenya walishiriki kupiga kura licha ya visa vya vurugu kuripotiwa katika baadhi ya sehemu za nchi ambapo takriban watu 15 wakiwemo polisi waliuawa .
Matokeo ya
mwanzo yanaonyesha Uhuru akiongoza kwa zaidi ya asilimia hamsini dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, 68.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa shughuli ya kuhesabu kura huenda ikaendelea hadi Jumatano kwa sababu ya idadi kubwa ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo.
Hatua hii nayo huenda ikachelewesha kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu.
Watu waliendesha shughuli hiyo kwa amani kwani ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya uchaguzi huu kwa hofu ya kutokea tena ghasia za kikabila zilizoshuhudiwa mwaka 2007.