London, England. Yaya Toure ameishtua klabu yake
ya Manchester City kwa kusema atakuwa tayari kuondoka Etihad, labda kama
atapewa mkataba mwingine kabla ya Jumamosi.
Nipewe mkataba mwingine, vinginevyo naondoka, alisema Toure kiungo tegemeo la Man City.
Kiungo huyo wa Ivory Coast amekasirishwa na ukimya wa mkataba wake
mpya ambapo mazungumzo yamekwama kwa muda wa miezi sita sasa.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk, alikiri kwa kusema: Kama atasaini
mkataba mpya ndani ya siku nne au tano, hiyo sawa. Kama hilo
halitatimia, hakutakuwa tena na muda wa kusubiri na tutaanza mazungumzo
na
klabu nyingine mara moja.
Tunataka watu wafahamu kinachoendelea kwenye klabu ili
uamuzi wake
wa kuondoka kama hatapewa mkataba mwingine basi iwe wazi, alisema.Leo ni Jumanne (juzi), kama mpaka Jumamosi hakutakuwa na mazungumzo
ya mkataba mpya, tutasema asante, Yaya ataondoka City Mei, alisema
wakala huyo. Aliongeza kwa kusema: Sidhani kama ataendelea kubaki Manchester
City. Siyo sababu ya pesa, anataka kuondoka kwa sababu kadhaa ndani ya
klabu.
Yeye ni mchezaji tegemeo kubwa Manchester City, lakini haoni kama
anaheshimika na wafanyakazi wa klabu. Roberto Mancini peke yake ndiye
anamuheshimu Yaya. Kiungo huyo wa zamani wa Timu ya Barcelona ya Hispania (29), ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi.
Man City inamlipa mshahara wake kwa wiki ni Pauni 220,000 tangu atue kutoka Barcelona.
Lakini wakala wake Seluk anasisitiza kwa kusema kwamba hajaomba
kuongeza pesa zaidi, lakini hafurahishwi na mambo yanavyokwenda ndani ya
klabu.
Kuna mambo hafurahishwi nayo, anataka kwanza yawekwe vizuri. Kwa sasa Toure, yuko na kikiso chake cha timu ya Taifa Ivory Coast
kinachocheza mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia
mwaka 2014 dhidi ya Gambia mwishoni mwa wiki hii.