
Pointi moja waliyoipata, iliwatosha kabisa
kuwafanya wawe
miongoni mwa timu 20 zitakazo pambana msimu ujao kusaka
ubingwa wa kombe la
ligi kuu nchini England,ligi yenye mashabiki wengi
duniani.
Hii
imekuwa mara ya kwanza kwa Cardiff kurejea kwenye ligi ya juu zaidi
nchini Uingereza baada ya miaka 51 ya kupambana kwenye ligi ndogo toka
waliposhuka daraja mwaka 1962.
Cardiff inakuwa timu ya pili kutoka nchi ya
Wales ambayo ni sehemu ya Taifa la Uingereza kushiriki ligi kuu baada ya
Swansea iliyopanda daraja misimu miwili iliyopita. Pia inakuwa timu ya
46 tofauti kushiriki ligi kuu nchini England toka ilipoitwa ligi kuu ya
England mwaka 1992.
Misimu mitatu iliyopita,Cardiff ilijitahidi
kupanda daraja lakini ilijikuta ikishindwa baada kutolewa kwenye michezo
ya mtoano,lakini msimu huu umekuwa wa mafanikio kwa klabu hiyo ambayo
inanolewa na kocha Malcolm George kutoka Scotland.
Mmiliki wa klabu ya Cardiff,Vincent Tan
Miaka mitatu iliyopita,wiki chache baada ya
kufungwa na Blackpool na kupoteza nafasi ya kwenda ligi kuu,Cardiff
ilijikuta kwenye matatizo makubwa baada ya kufikishwa mahakamani mara
tatu baada ya kushindwa kulipa deni la malimbikizo ya kodi. Lakini deni
hilo lilikuja kulipwa lote kwa pamoja na Bilionea Vincent Tan kupitia
kampuni yake ya Malaysian Consortium ya Malaysia,ambayo iliwekeza kiasi
cha paundi milioni 60 kwenye klabu hiyo.
Timu nyingine zitakazopanda daraja msimu ujao
kwenye ligi ya Uingereza na zile zitakazoshuka kutoka ligi kuu kwenda
ligi ya chini zitajulikana mwishoni mwa mwezi ujao.