![]() |
Kocha wa Chelsea - Rafael Benitez |
Pongezi kwa Fernando Torres ambaye alifunga mara mbili na shambulizi la hatari kutoka kwa Victor Moses, wa Russia hao walipata goli la ugenini kwa mkwaju wa penati ya Bibras Natcho. Licha ya kukiri kutokuwa na furaha, Mhispania huyo aliridhika na matokeo na kutarajia kuwa timu yake itapata ushindi katika mchezo wa marudiano.
"Ni dhahiri, wanatakiwa kufunga magoli mawili, nawanaweza kwenda kama tusipofunga, lakini tunajiamini tunaweza kufunga," Benitez
aliwaambia waandishi wa habari. "Ninafuraha lakini si kwa asilimia 100 kwasababu tumekubali kufungwa goli wakati tulikuwa katika udhibiti wa mchezo. Nafikiri penati ilikuwa mbaya. Tukio lilikuwa mbali mno kuweza kuona kwa uwazi lakini lilikuwa limechanganywa na maamuzi ya muamuzi, japokuwa yalikuwa sehemu ya mchezo.
"Mimi nilikuwa radhi kuona timu inashinda, Fernando yeye alikuwa anafanya kazi vizuri katika mafunzo na sisi tulikuwa na furaha na mchango wake kwa timu na kiwango cha kazi na si tu kwa goli"
Mabao mawili yaTorres yamemfanya mshambuliaji huyo afikishe magoli 18 katika mashindano yote msimu huu na Benitez alifurahishwa na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa kazi nzuri na yenye uhakika."Fernando amefunga baadhi ya magoli na nina uhakika kwamba atafunga menginezaidi, "alisema.
![]() |
Fernando Torres - muuwaji aliyeiuwa Rubin Kazan. |
"Nadhani kwamba Fernando anahitajika kufunga goli kwasababu kila mkutano na waandishi mimi hujibu maswali kadhaa. Leo tuliona kwamba anaweza kufanya kazi kwa bidii,kimwili yukosawa na ninatumaini kwamba anaweza kuendelea na kufunga mabao hadi mwisho wa msimu. "Washambuliaji huwa wanatakiwa kufunga mabao, na wakifanya hivyo, kujiamini kutakuwa huko kutoka mwanzo. Nilikuwa na shaka kuhusu Fernando, na ujasiri wake sasa umeongezeka na tunaweza kuona kwamba pamoja na kupitia kila pasi."
Pamoja na Chelsea kucheza michezo mitatu kwa siku sita, Benitez alithibitisha kuwa ataendelea na mzunguko katika kikosi chake kabla ya mpambano wao wa ligi kuu dhidi ya Sunderland siku ya Jumapili.
"Lengo letu ni juu ya mchezo wetu ujao, ni matumaini yangu kuwa tunaweza kushinda dhidi ya Sunderland na kwamba itakuwa ushindi wa tatu wiki hii," alisema. "Tunajua kwamba itakuwa vigumu lakini bado nina imani kwamba tunaweza kusimamia kikosi na kuendelea mpaka mwisho.
"Mabadiliko hutegemea kila mchezaji; si mimi tu kufikiri kufanya hili au lile. Unatakiwa kuangalia kila mchezaji na jinsi walivyo ni safi. "Sijui ni wangapi lakini sisi tunatakiwa kuwa na mabadiliko ya wachezaji kila mchezo. na kipaumbele chetu sasa ni dhidi ya Sunderland na mchezo huo ambao pia huathiri uteuzi wetu kwa mechi ya pili.".