Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ataondoka kwenye kibarua cha kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Rais wa klabu ya Real
Madrid,Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari jumatatu jioni kuwa
Mourinho hatofukuzwa bali wamekubaliana kumaliza mkataba wao na kocha huyo raia
wa Ureno.
Aidha Madrid,
imeongeza kuwa haijaanza mazungumzo na kocha yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi
ya Mourinho lakini vyanzo mbalimbali vya habari za michezo zinamtaja kocha wa
PSG ya Ufaransa, Carlo Ancelloti kuchukua jukumu la kuifundisha Madrid msimu
ujao.
Duru za kimichezo
zinasema, Jose Mourinho huenda akarejea nchini Uingereza kuifundisha klabu yake
ya zamani ya Chelsea baada ya kuwepo makubaliano baina yake na uongozi wa klabu
hiyo.
BBC.