Thursday, July 4

Rais Kikwete awashukuru Wananchi kwa ushirikiano mzuri ziara ya Obama

Raisi Jakaya Kikwete awashukuru wananchi kwa kuonyesha ushirikiano katika ziara ya siku mbili ya Rais wa Marekani, Barack Obama wakati alipokuwa nchini.Ikiwemo na kuvishukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano mzuri wa matukio yote wakati wa ugeni huo mzito wa mulululizo uliofika nchini kuwajulisha watanzania 

Ikiwemo na ushirikiano ulioonyeshwa wakati wageni wengine waliokuja nchini kushiriki mikutano ikiwemo na ujio wa Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na mkewe Mama Laura Bush kuja kushiriki mkutano pamoja na wake wa marais wa Afrika 

Wake wa marais waliyohudhuria mkutano huo na mstaafu huyo ni pamoja na yule wa Afrika ya Kusini, Ethiopia, Mozambique, Ghana, Sierra Leone na Uganda. 

Rais Kikwete pia hakusita kuvishukuru vyombo vya ulinzi, taasisi za kibiashara na makampuni mbalimbali kwa mchango waliouonesha kufanikisha shughuli za ugeni 

“Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wananchi wote, hasa wale wakazi wa Dar es Salaam, Kwa kuonyesha ukarimu, uvumilivu na utulivu mkubwa wakati wote wa matukio hayo” 

“Nathubutu kwa kusema najivunia sana ushiriki wenu katika shughuli zote za kitaifa kwani natambua mazingira yalivyokuwa wakati wa ugeni huo, mmeijengea nchi yetu heshima kubwa.” Asanteni sana 

Hata hivyo baadhi ya wakazi waliopata kuzungumza na mtandao huu waliilalamikia serikali kwa kitendo cha kuwanyima uhuru kwa kumuona kiufasaha Rais Obama kwa kukosa fursa ya kutokumuona vizuri ikiwemo kukimbiza msafara kwa kasi kubwa hali ambayo wengi waliilalamikia 

“Tumesikitishwa sana, sisi tulitarajia huyu kipenzi chetu tungepat fursa nzuri tu lakini walimpitisha kiwa mwendo kasi, tunaomba safari nyingine wampitishe katika gari la wazi tumfaidi vizuri” walilalama wakazi hao 

Ziara ya Rais Obama ilipokelewa kwa shangwe sana kwa watanzania kwani watu wengi walijitokeza huku wengine walifunga ofisi na kujipanga barabara kuangalia msafara wakati wa kuja na wakati alipokuwa akiondoka nchini hali iliyoashiria wengi walifurahia ujio wa Rais huyo wa Marekani.