Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amefika mahakamani ambapo ameshtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake.
Mahakama imemsomea makosa ya kumuua,Reeva Steenkamp. Kesi dhidi ya mwanariadha huyo itaanza Mwezi Machi mwaka ujao.Kesi hiyo sasa imehamishiwa mahakama kuu na itasikizwa mapema mwakani.Pistorioua anadaiwa kumpiga risasi mpenzi wake usiku wa manane akiwa amejifungia choo ya nyumba yake.
Mwanariadha huyo amejitetea na kusema alidhania ni mtu mwingine aliyejaribu kuingia kwa nguvu ndani ya nyumba. Upande wa mashtaka umesema mwanariadha huyo alipanga kumuua mwanamitindo huyo.
Mmoja wa majirani wa Pistorius na ambaya ni shahidi alikiri kusikia mayoye ya mwanamke kisha milio ya risasi. Hata hivyo shahidi mkuu anayefahamu kilichotokea wakati huo ni mmoja tu naye ni Oscar Pistorius.
Chanzo: bbc