Fabius amesema hayo siku moja baada ya Marekani na Urusi kuweka uzito katika mazungumzo hayo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu, ambayo Umoja wa Mataifa umesema hatimaye yatafanyika Januari 22. Mpatanishi wa kimataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi amesema orodha ya washiriki haijapangwa. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Romain Nadal amesema Ufaransa inataka pande zote kutuma ujumbe mmoja kila mmoja.