Nguchiro:
Nguchiro ni wanyama wadogo kiasi wa familia Herpestidae. Kuna spishi nne huko Madagaska ziitwazo nguchiro pia na ambazo ziliainishwa katika Herpestidae, lakini malinganisho ya ADN yameonyesha kwamba spishi hizi zina mnasaba zaida na spishi za Eupleridae. Sasa zimepewanusufamilia yao binafsi Galidiinae. Nguchiro wa kweli wanatokea Afrika, Asia na Ulaya ya kusini. Wamewasilishwa katika visiwa kadhaa vya Karibi naHawaii ambapo wamekuwa usumbufu.
Wanyama hawa ni warefu na wembamba na wana mkia mrefu wenye manyoya mengi. Wanafanana na chororo lakini wako wakubwa zaidi. Rangi yao ni hudhurungi, kahawia, kijivu au nyeusi. Wao ni wanyama mbua na hula wadudu, kaa, nyungunyungu, mijusi, nyoka, ndege na wagugunaji, na mara nyingi mayai na mizoga pia. Nguchiro hujulikana kwa uwezo wao wa kuua nyoka na kukinga sumu yao. Huishi peke yao au kwa makundi (k.m.nguchiro miraba na nguchiro-jangwa) na hukiakia mchana lakini pengine usiku pia.
Spishi za Afrika:
- Atilax paludinosus, Nguchiro-maji (Marsh Mongoose)
- Bdeogale crassicauda, Nguchiro Kijivu (Bushy-tailed Mongoose)
- Bdeogale jacksoni, Nguchiro wa Jackson (Jackson's Mongoose)
- Bdeogale nigripes, Nguchiro Miguu-myeusi (Black-footed Mongoose)
- Bdeogale omnivora, Nguchiro-pwani (Sokoke Bushy-tailed Mongoose)
- Crossarchus alexandri, Nguchiro wa Alexander (Alexander's Kusimanse)
- Crossarchus ansorgei, Nguchiro wa Angola (Angolan Kusimanse)
- Crossarchus obscurus, Nguchiro Magharibi (Common Kusimanse)
- Crossarchus platycephalus, Nguchiro Kichwa-kipana (Flat-headed Kusimanse)
- Cynictis penicillata, Nguchiro Njano (Yellow Mongoose)
- Dologale dybowskii, Nguchiro wa Pousargues Pousargues's Mongoose)
- Galerella flavescens, Nguchiro Mwembamba wa Angola (Angolan Slender Mongoose)
- Galerella nigrata, Nguchiro Mweusi (Black Mongoose)
- Galerella ochracea, Nguchiro Mwembamba Somali (Somali Slender Mongoose)
- Galerella pulverulenta, Nguchiro Kusi (Cape Gray Mongoose)
- Galerella sanguinea, Nguchiro Mwembamba Slender Mongoose)
- Helogale hirtula, Nguchiro Mdogo Somali au Kitafe Somali (Somali Dwarf Mongoose)
- Helogale parvula, Nguchiro Mdogo wa Kawaida au Kitafe wa Kawaida (Common Dwarf Mongoose)
- Herpestes ichneumon, Nguchiro Mkubwa (Egyptian Mongoose)
- Herpestes naso, Nguchiro Pua-ndefu (Long-nosed Mongoose)
- Ichneumia albicauda, Nguchiro Mkia-mweupe (White-tailed Mongoose)
- Liberiictis kuhni, Nguchiro wa Liberia (Liberian Mongoose)
- Mungos gambianus, Nguchiro wa Gambia (Gambian Mongoose)
- Mungos mungo, Nguchiro Miraba (Banded Mongoose)
- Paracynictis selousi, Nguchiro wa Selous (Selous' Mongoose)
- Rhynchogale melleri, Nguchiro wa Meller (Meller's Mongoose)
- Suricata suricatta, Nguchiro-jangwa (Meerkat)
Spishi za mabara mengine:
- Herpestes brachyurus, Nguchiro Mkia-mfupi) (Short-tailed Mongoose)
- Herpestes edwardsii, Nguchiro Kijivu wa Uhindi (Indian Gray Mongoose)
- Herpestes fuscus, Nguchiro Kahawia wa Uhindi (Indian Brown Mongoose)
- Herpestes javanicus, Nguchiro Mdogo wa Asia (Small Asian Mongoose)
- Herpestes semitorquatus, Nguchiro Koo-jeupe (Collared Mongoose)
- Herpestes smithii, Nguchiro Uso-mwekundu (Ruddy Mongoose)
- Herpestes urva, Nguchiro Mlakaa (Crab-eating Mongoose)
- Herpestes vitticollis, Nguchiro Shingo-milia (Stripe-necked Mongoose)