Thursday, February 20

Arsenal yafungwa 2-0 nyumbani.

Timu za Uingereza zimezidi kuandikisha matokeo mabaya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal ilipigwa mabao mawili kwa bila na Beyern Munich ya Ujerumani katika mchuano wa robo fainali. Arsenal ililazimika kuwachezesha wachezaji kumi pekee uwanjani baada ya mlinda lango wake kuonyeshwa kadi nyekundu.
Mchezaji Mesut Ozil alipoteza penalti ya Arsenal katika kipindi cha kwanza sawa na David Alaba aliyeshindwa kufunga penalti ya Bayern Munich.
Hii inatokea baada ya Manchester City kuchapwa mabao mawili kwa bila Jumanne na Bercalona ya Uhispania. Timu nyingine za Uingereza ambazo ziko katika kinyang'anyiro hicho ni Chesea na Manchester United ambazo zitacheza michuano hiyo baadaye mwezi ujao.
Katika mechi nyingine iliyochezwa hapo jana Atletico Madrid ya Uhispania iliishinda AC Millan ya Italia bao moja kwa bila na ikiwa itasonga mbele hii itakuwa mara ya kwanza Atletico Madrid kuingia robo fainali tangu mwaka 1997.

Chanzo: bbc

Wednesday, February 19

Man City yaduwazwa nyumbani na Barcelona.

Matumani ya timu ya Manchester City kunyakuwa taji la ligi ya mabingwa ulaya yalipata pigo baada ya wachezaji wa Barcelona Lionel Messi na Dani Alves kufunga jumla ya mabao mawili katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Etihad.
Messi alikuwa wa kwanza kufunga kupitia penalty katika dakika ya 54 alipoangushwa na difenda Martin Demichelis aliyepewa kadhio nyekundu.
Licha ya Manchester City kuwa kasoro mchezaji mmoja walijizatiti kukabiliana na timu hiyo ya Uhispania ila Dani Alves alizima matumaini yao mbele ya mashabiki wao alipofunga bao la pili mwisho mwisho wa kipindi cha pili.
Ili kuingia robo fainali itahithitajika kuichapa Bercalona mabao matatu kwa bila.
Katika mechi nyingine ya timu hizo kumi na sita, nchini Ujerumani Bayer Liverkusen iliicharazwa mabao mane kwa bila na Paris Saint Germain ya Ufaransa. Mabao matatu yalifungwa kipindi cha kwanza na la nne katika kipindi cha pili.
Leo Arsenal ambao wako katika nafasi ya pili kwenye ligii ya Uingereza itacheza dhidi ya bingwa mtetezi wa kombe hilo Beyern Munich wakati AC Millan ya Italia itakuwa ikipambana Atletico Madrid ya Uhispania.

chanzo: bbc

Unamjua Nguchiro?

Nguchiro:


Nguchiro ni wanyama wadogo kiasi wa familia Herpestidae. Kuna spishi nne huko Madagaska ziitwazo nguchiro pia na ambazo ziliainishwa katika Herpestidae, lakini malinganisho ya ADN yameonyesha kwamba spishi hizi zina mnasaba zaida na spishi za Eupleridae. Sasa zimepewanusufamilia yao binafsi Galidiinae. Nguchiro wa kweli wanatokea AfrikaAsia na Ulaya ya kusini. Wamewasilishwa katika visiwa kadhaa vya Karibi naHawaii ambapo wamekuwa usumbufu.
Wanyama hawa ni warefu na wembamba na wana mkia mrefu wenye manyoya mengi. Wanafanana na chororo lakini wako wakubwa zaidi. Rangi yao ni hudhurungi, kahawia, kijivu au nyeusi. Wao ni wanyama mbua na hula wadudukaanyungunyungumijusinyokandege na wagugunaji, na mara nyingi mayai na mizoga pia. Nguchiro hujulikana kwa uwezo wao wa kuua nyoka na kukinga sumu yao. Huishi peke yao au kwa makundi (k.m.nguchiro miraba na nguchiro-jangwa) na hukiakia mchana lakini pengine usiku pia.

Spishi za Afrika:



Spishi za mabara mengine:

Mjue ndege aina ya Mbuni.

UTANGULIZI:



Mbuni ni ndege wakubwa, huku asili yao ikiwa ni Afrika. Hawa ni ndege wasio na uwezo wa kuruka. Wanapatikana kwenye oda ya Struthioniformes, pamoja na ndugu aitwaye kiwi. Mbuni ni wa pekee sana sababu ya muonekane wake, wa shingo na miguu mirefu pamoja na uwezo wake mkubwa wa kukimbia, karibu ya maili 45 kwa saa. Huu ni mwendokasi mkubwa zaidi kwa ndege yeyote ardhini. Mbuni ndiyo ndege mkubwa kuliko wote wanaoishi duniani, wakiwa pia ndio watagaji wa mayai makubwa kuliko wote pia.

Mlo wa mbuni kwa kiasi kikubwa huwa ni mimea, ingawa pia hula wadudu. Mbuni huishi katika makundi ya kutansatanga kati ya ndege watano mpaka hamsini. Wanapotishwa, mbuni hujificha kwa kulala ardhini au kukimbia mbali kama wakizingirwa, hushambulia adui zao kwa miguu yao yenye nguvu. Tabia kujamiiana hutofautiana kutoka maeneo moja mpaka vingine, ambapo mbuni dume hupigaia mbani jike hupigania nafasi ya kuwapata mbuni jike kwa nguvu.
Mbuni hufugwa dunia nzima, hasa kutokana na manyoya yake, ambayo hunitia na kutumika kuondolea vumbi. Ngozi yake hutumika kutangenezea mtu mbali mbali huku nyama yake ikilizwa kibiashara.

MAELEZO:


Mbuni huwa na uzito wa kilogramu 63-130, luku mbuni dume wakifika mpaka uzito wa kg 155. Manyoya ya mbuni dumu wakubwa huwa kwa kiasi kikubwa meusi huku mkia ukiwa wakubwa huwa na rangi ya kahawia na nyeupe. Vichwa vya mbuni wote huwa havina manyoya. Ngozi za mbuni jike huwa na rangi ya pinki – kijini, huku dume wakiwa na ngozi ya bluu au kijini kutegemeana na nususpishi.

Shingo zao ndefu, hukiweka kichwa chao mita 1.8 mpaka 2.75 juu ya ardhi, na macho yao husemwa kuwa ndiyo makubwa kuliko wanyama wote wa ardhini, yakiwa na sm 5, hivyo huweza kuwaona adui zao hata wakiwa mbali sana. Macho yao yanakingwa na mwanga mkali wa jua kutoka juu.

Miguu ya mbuni, kama ilivyo kwa ndege wengine, haina manyoya isipokuwa magamba. Ndege hawa wawili huwa na vidole vikubwa viwili huku wengi wakiwa na vine, huku kucha moja ikiwa kubwa, ikifanana na kwato. Mbawa hutanuka kwa upana wa mita 2 hivyi, na hutumika sana kwenye tabia za kujamiiana na kujikinga na jua. Wana manyoya 50-60 hivi ya mkiani. Midomo yao huwa mipana na ncha ya duara kidogo. Tofauti na ndege wengine, mbuni hutoa mkoja tofauti na kinyesi, hivyo kuwa na kibofu. Pia tofauti na ndege wengine tena, huwa na ogani ya kutolea manii inayoweza kutoka nje ya mwili kwa urefu wa inchi 8.
Mbuni hukomaa na kuwa na uwezo wa kuzaa wakiwa na miaka miwili/minne watoto wa mbuni hukua kwa kiasi ya sm 25 kwa mwezi. Wakiwa na umri wa mwaka mmoja tu, mbuni huwa na uzito wa kg 45. Mbuni jike huweza kuyatambua mayai yake hata kwenye kiota cha jumuiya.

UZAZI:



Kujamiiana huwa na misimu tofauti kutokana na maeneo. Mbuni dume hupigania nafasi ya kujamiiana na jike wengine, na akishinda basi huwa na uwezo wa kujamiiana na jike wote wa kundi lake lote japo atakuwa na jike wake atakayedumu naye kwa wakati husika.

Mbuni dume humvutia mbuni jike, kwa kumchezeachezea na kumpigia mbawa zake, ambaye humfuata na wao huenda faragha kwa ajili ya kujamiiana. Wakifika huko huwafukuza wanyama/mbuni wengine kama wapo na kisha dume kuweza tena, mbuni jike hukaa chini na kuwa tayari kwa kujamiiana.
Mbuni jike hutaga mayai yaliyorutubishwa kwenye kiota cha jumuiya, ambacho huwa ni shimo lenye upana wa mita tatu na kina cha sentimeta 30-60. Mbuni dume ndiyo huchimba kiota hiki mayai ya mbuni ndiyo mayai makubwa kuliko yote na huwa na uzito wa kg 1.4, zaidi ya mara 20 ya yai la kuku. Huwa na rangi ya maziwa na wakati mwingine pamoja na madoa madogo. Mayai hutumiwa na mbuni jike wakati wa mchana na kutamiwa na mbuni dume wakati wa usiku . Mayai huanguliwa baada ya siku 35-45, na kisha hapo mbuni jike na dume wote hushirikiana kuwakuza watoto wao. Mbuni weusi huwindwa wakati huu, na mara nyingi mbuni mtoto mmoja tu ndiyo hufanikiwa kukua, huku wengine wakigeuzwa kitoweo na wanyama wengine wala nyama. Mbuni wanaokuzwa na binadamu, huhamisha sana upendo wao, na kuanza kuwapenda sana binadamu wanaowatunza.

SPISH:



.

Monday, January 20

Chelsea yaiadhibu Man U.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa matumaini ya mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Premier, Manchester United ya kulihifadhi kombe hilo msimu huu yametumbukia nyongo, baada ya klabu yake kuishinda United kwa magoli matatu kwa moja.
Nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o aliifungia Chelsea magoli yote matatu na kuandikisha historia yake ya kufunga magoli matatu katika mechi moja ya ligi kuu ya Premier.
Chelsea hata hivyo imesalia nafasi ya tatu alama mbili nyuma ya Arsenal na moja nyuma ya Manchester City.

Mourinho amesema itakuwa rahisi kwa ngamia kuingia tundu la sindano kuliko Manchester United kushinda taji la ligi kuu msimu huu.

'' Ni vigumu sana. Wao wana alama kumi na nne nyuma ya Arsenal, kumi na tatu nyuma ya Manchester City na kumi na mbili nyuma yetu'' Alisema Mourinho.
''Pengine timu moja isambaratike, lakini kwa timu tatu kusambaratika kwa pamoja, itakuwa vigumu sana. Nadhani kilichosalia ni wao kupigania kumaliza katika nafasi za kwanza nne'' Aliongeza Mourinho.
Kadi Uwanjani
Nahodha wa United Nemanja Vidic alipewa kadi ya njano muda mfupi kabla ya mechi hiyo kumalizika, baada ya kumfanyia madhambi Eden Hazard, naye Rafael da Silve akaonyeshwa kadi ya njano kwa kumjeruhi Gary Cahili dakika moja baadaye.
Hata hivyo kocha wa Manchester United, Moyes, alihisi kuwa refa wa mechi hiyo alichukua uamuzi mkali zaidi kwa kumpa Vidic kadi nyekundu ya moja kwa moja, huku akikiri kuwa Rafael alikuwa na bahati sana pale refa alipompa kadi ya njano badala ya kadi nyekundu.

Naye Mourinho alimsifu Eto'o mwenye umri wa miaka thelathini na mbili, licha ya kuwa aliwahi kumshutumu kuhusiana na matokeo yake hasa baada ya kuwasili kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala mapema msimu huu.

Chanzo bbc

Friday, December 6

Droo ya Kombe la dunia 2014 Brazil:

Itafanyika wapi? Costa do Sauipe, Bahia, Brazil
Kombe la dunia la mwaka 2014, linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 12 Juni hadi Julai kumi na tatu.

Ijumaa hii mbivu na mbichi itajulikana na itakuwa itakuwa wakati wa kujua nani atacheza na nani katika kundi gani droo zitakapofanyika.Itakuwa mara ya 20 kwa kinyang’anyiro hicho kuandaliwa huku ikiwa mara ya kwanza kufanyika nchini Brazil tangu mwaka 1950 wakati wenyeji waliposhindwa na Uruguay kwenye fainali.
Droo yenyewe itafanyika kuanzia saa moja jioni saa za Afrika Mashariki Ijumaa tarehe sita.
Itafanyika mjini Costa do Sauipe mkoani Bahia, umbali wa maili 56 kutoka mjini Salvador, mji utakaokuwa mwenyeji wa kombe hilo.
Wakati wa droo kutakuwa makundi manne
La kwanza likiwa na timu hizi: Brazil, Spain, Argentina, Belgium, Colombia, Germany, Switzerland, Uruguay.
Kundi la pili: Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria, Cameroon, Chile, Ecuador.
Kundi la tatu: Japan, Iran, South Korea, Australia, United States, Mexico, Costa Rica, Honduras.
Kundi la nne: Bosnia-Hercegovina, Croatia, England, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, France.
Watakaofanya droo ni mchezaji wa zamani wa England Sir Geoff Hurst, Zinedine Zidane wa Ufaransa, Cafu wa Brazil na Fabio Cannavaro wa Italia.
Timu 32 zilizofuzu zitawekwa katika makundi manane kila kikundi kikiwa na timu nne.

Chanzo: bbc.

Thursday, December 5

Mzee Nelson Mandela afariki dunia.

Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.

Chanzo: bbc.