![]() |
Jaji mkuu wa Kenya, Willy Mutunga. |
Jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga, ameelezea kuwa alipokea vitisho hivi karibuni kuhusu kesi iliyowahusisha mgombea wa urais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.
Wawili hao ni washukiwa wa
uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC na mahakama kuu ya Kenya wiki jana ilipaswa kuamua ikiwa wanaweza kugombea urais au la.Jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa ujumbe wa barua aliyopkea ulikuwa unamtisha kuwa angetendewa jambo baya na kundi haramu la Mungiki.Uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo hata hivyo ulisema kuwa haina uwezo wa kuamua kesi hiyo na kwamba mahakama ya juu zaidi Kenya ndiyo ina uwezo pekee kutoa uamuzi.
Kundi hilo pia lilihusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007.
Mutunga aliituhumu serikali kwa kumfanyia dhulma baada ya kuamrishwa na afisaa mmoja wa uhamiaji kusafiri kwenda Dar es Salaam kwani hakuwa na idhini ya mtumishi mkuu wa umaa Francis Kimemia.
Bwana Mutunga alisema hatishiki na kuwa hahitaji idhini kutoka kwa Kimemia kabla ya kusafiri kwenda nje ya nchi.
Pia ameelezea wasiwasi kuwa majaji wanatishwa kisiasa huku nchi ikiwa inaelekea katika uchaguzi mku