![]() |
Hamadi Jebali - Waziri mkuu wa tinisia aliye jiuzulu. |
Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali, amejiuzulu baada ya kushindwa kuafiki makubaliano kuhusu serikali mpya.
Bwana Jebali,alikuwa anajaribu kuunda serikali
mpya kufuatia msukosuko wa kisiasa uliosababishwa na mauaji ya
mwanasiasa wa upinzani Chokri Belaid wiki mbili zilizopita.Awali alisema alikuwa tayari kujiuzulu ikiwa chama chake cha kiisilamu cha Ennahda hakingeunga mkono mpango wake wa kuwateua wataalamu kama wanachama wa baraza la mawaziri.
Mauaji ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika Februari sita, yalisababisha maandamano na ghasia pamoja na kujiuzulu kwa maafisa wa
serikali.
''Niliapa kuwa ikiwa mpango wangu haungefaulu, ningejiuzulu, na nimefanya hivyo,'' alisema bwana Jebali baada ya kukutana na rais Moncef Marzouki.
Akitaja hatua yake kama jambo la kusikitisha , alisema aliamua kujiuzulu ili kutimiza ahadi yake kwa wananchi wa Tunisia.
"watu wetu wana ndoto fulani, ambazo wanataka wanasiasa kuwatimizia. Lazima tuweze kuwaweka imani watu wetu,'' alisisitiza Jebali.
Na aliongeza kuwa, kukosa kufaulu kwa mpango wangu, haina maana kuwa Tunisia imefeli, au mapinduzi hayakuwa na faida,'' akigusia mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika miaka miwili iliyopita ambapo rais wa zamani Zine al-Abidine Ben Ali alipinduliwa.
HBARI NA BBC.