![]() |
Kikosi cha JKT Oljoro ya Arusha. |
MABINGWA wa soka Simba jana wameendelea taratibu kutoka nje ya mstari wa mbio za ubingwa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Matokeo hayo yaliwakera mashabiki wa Simba, ambao
waliwazomea wachezaji wao mara baada ya mchezo, huku pia wakiimba
‘Okwi..Okwi...Okwi.’
Hiyo ni sare ya pili mfululizo, ambapo wiki
iliyopita ililazimishwa sare kama hiyo na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa
Taifa. Simba sas
a imefikisha pointi 28 na kuendelea kuwa nyuma ya mahasimu wao Yanga wanaoongoza kwa kuwa na pointi 30, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
a imefikisha pointi 28 na kuendelea kuwa nyuma ya mahasimu wao Yanga wanaoongoza kwa kuwa na pointi 30, huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Azam inayoshuka dimbani leo, inashika nafasi ya
pili na kama itashinda basi itafikisha pointi 30, sawa na Yanga na hivyo kuongoza pamoja msimamo.
pili na kama itashinda basi itafikisha pointi 30, sawa na Yanga na hivyo kuongoza pamoja msimamo.
Katika mchezo huo, timu zote zilishambulia kwa
zamu, huku Simba waking’ara zaidi kipindi cha kwanza na wapinzani wao
wakiibuka kipindi cha pili.
![]() |
Kikosi cha Simba SC ya Dar-es-Salaam |
Wakati Simba wakipata sare hiyo, habari toka ndani
zinadai kuwa, wachezaji wa timu hiyo hawajalipwa mishahara ya
Januari.Mwananchi ilipomuuliza Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey
Nyange kuhusu madai hayo, alisema: “Hakuna kitu kama hicho Simba.”
Lakini pia Mwenyekiti, Aden Rage alipoulizwa
kuhusu suala hilo, alikuwa mkali na kumtaka mwandishi amtafute msemaji
wa Simba aongee. Mabingwa watetezi, Simba walikuwa wa kwanza kufunga bao
kupitia kwa kiungo Mwinyi Kazimoto katika dakika ya saba kwa shuti kali
nje kidogo ya eneo la hatari.
Wenyeji walisawazisha bao hilo dakika ya 55
kupitia kwa Paul Nonga aliyefunga kirahisi baada ya kuwazidi ujanja
Shomari Kapombe na Keita.
Oljoro nusura wafunge bao la pili katika dakika ya
78 kama siyo shuti kali la Salum Mbonge kupotea njia na kwenda kugonga
mwamba wa Simba.
Kihemba naye aliinyima Simba bao baada ya kupaisha
juu mpira akiwa ndani ya 18 za Oljoro kufuatia pasi nzuri kutoka kwa
mshambuliaji Ngasa.
![]() |
Mishemishe zilivyokuwa uwanja wa shekhe Amri Abeid Arusha. |
Kocha Patrick Liewig alimpumzisha Keita na kuingia
Edward Christopher (75), Rashid Mkoko na kuingia Mrisho Ngasa. Baada ya
mchezo, Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwehlo alimlalamikia mwamuzi
kwa kuinyima timu yake penalti.
Kwa upande wake, Katibu wa Oljoro, Alex Mwamgaya
alisema kikosi chao kilicheza vizuri na hiyo inatokana na wachezaji
kujituma uwanjani. Sare hiyo ya JKT Oljoro imewafikisha pointi 21, sawa
na Kagera Sugar yenye mchezo mmoja mkononi.