![]() |
Mo Farah. |
Mshindi wa dhahabu katika mbio za mita elfu kumi na
tano wakati wa michezo ya olimpiki Mo Farah, ametangaza kuwa atashiriki
katika mbio za mwaka huu za London Marathon.
Hata hivyo Farah, amesema kuwa atashiriki katika
mbio za maili 26.2 na wala sio mbio ndefu, huku akijiimarisha katika
mbio za mita elfu tano na kumi.Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29, ameiambia BBC kuwa atashiriki katika mbio masafa marefu mwaka ujao.
Lakini aliyekuwa bingwa wa mbio hizo kwa kina dada Paula Radcliffe, amehoji uamuzi wa mwanariadha huyo.
Radcliffe, mbio za London marathon mwaka wa 2002, 2003 na 2005, amesema uamuzi huo sio wa busara akisema kuwa ni vyema mwanariadha huyo
kuangazia mbio za mita elfu tano na kumi badala ya kutapatapa.
Farah hii leo ameanza msimu wake kwa kuandikisha ushindi katika mbio za mita elfu tatu wakati wa mashindano ya riadha ya ndani mjini Birmingham.
Ripoti zinasema kuwa Farah atashiriki katika mbio za kilomita 21 mjini New Orleans wiki ijayo.
Hata hivyo Farah atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mshikilizi wa rekodi ya ulimwengu katika mbio hizo mkenya Patrick Makau, bingwa wa olimpiki Stephen Kiprotich na bingwa wa ulimwengu Abel Kirui.