Sunday, February 17

Kenya yalaani madai ya al-Shabaab kumuua mateka wa Kenya

Serikali ya Kenya siku ya Ijumaa (tarehe 15 Februari) iliilaani al-Shabaab kwa madai yake ya kumuua mwanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) katika kizuizi chao, wakati kikundi cha wapiganaji kimetishia kuwaua Wakenya wengine watano kama madai yao hayakutimizwa.
"Ingawa madai hayo hayawezi kuthibitishwa, KDF inalaani vikali tuhuma za mauaji", msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir alisema katika Twitter siku ya Ijumaa.
Chirchir alisema vitisho vya ziada vya kuwaua mateka zaidi Wakenya vinaonyesha kuendelea na kutojali kwa al-Shabaab kuhusu maisha na
hadhi ya watu. "KDF inaendelea kuahidi kulinda usalama na kudhoofisha uwezo wa Al Shabaab kuvuruga amani na utulivu wa kanda" Chirchir alisema.
Al-Shabaab awali walitishia kuwaua Wakenya hao
sita chini ya umiliki wao katika ujumbe wa video tarehe 23 Januari, wakidai kuachiwa kwa Waislamu wote walioshutumiwa kwa ugaidi katika gereza la Wakenya, pamoja na kuwaachia huru Waislamu waliorejeshwa kuhukumiwa Uganda kwa kesi ya ugaidi, kwa kurejelea udhahiri wa wale waliofungwa kwa kesi ya al-Shabaab kulipua bomu mwaka 2010 huko
Kampala lililoua watu 74.
Video hiyo iliipa serikali wiki tatu kuwaachia huru, sharti ambalo liliisha siku ya Alhamisi. Uchunguzi zaidi wa video ulionyesha kwamba al-Shabaab walikuwa waliwawakilisha visivyo mateka hao kama wafungwa wa vita, wakati kimsingi walikuwa wafanyakazi wa serikali.
Al-Shabaab waliipa serikali ya Kenya siku nyingine tatu kujibu madai yao. "Licha ya Wanajihadi kufungua milango ya mazungumzo na kuwapa muda mwingi, serikali ya Kenya imekuwa na uzembe wa makusudi na kushindwa kuchukua hatua zinazofaa kulinda uachiwaji huru wa wananchi wake," ilisema al-Shabaab katika taarifa.
"Katika masaa 72, wafungwa ama watapoteza maisha yao kwa sababu ya usaliti wa serikali yao au watasherehekea msaada wa serikali yao na kufurahia uhuru wao," kikundi hicho kilisema.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Yussuf Haji alisema kuwa kikundi hicho kinapaswa kuwaachilia bila masharti maafisa wawili wa serikali waliowateka huko Wajir mwezi Januari 2011.
"Bado nina msimamo wa kuwa kikundi hicho kinapaswa kuwaachia huru raia iliyowateka kutoka Kenya ili waweze kuungana na familia zao. Katika hali ya vita, hakuna upande ambao utakamata raia ili kuwatumia kwa madai yoyote," aliiambia Sabahi.
Alisema kuwa uuaji wa mateka unakatazwa katika Uislamu, dini ambayo kikundi kinadai kuifuata.
Adan Yussuf Muse, mshauri wa usalama anayeishi Nairobi, aliiambia Sabahi kuwa kwa vile ni vigumu kukubali iwapo madai ya kuwanyonga ni kweli, wanamgambo walijifunza kutokana na makosa yao ya nyuma kwa kutuonesha picha za maafisa walio waua.
"Tofauti na kabla, wakati ilipokuwa ikituma ujumbe katika akaunti yao ya Twitter, kikundi kiliamua kutuma ujumbe kwa vyombo vya habari, pengine kwa hofu kwamba akanuti yao mpya ingeweza kufungwa kama ilivyokuwa ya kwanza," Muse alisema