Sunday, February 17

Wagombea urais wa Kenya wafanya mdahalo wa kwanza wa kipekee.

Wagombea urais nane wa Kenya walifanya mdahalo wa kwanza wa kipekee wa ana kwa ana siku ya Jumatatu (tarehe 11 Februari) wakati wasiwasi ukiukumba uchaguzi wa mwezi ujao.
Wagombea -- Waziri Mkuu Raila Odinga, Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta, Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi, mbunge Martha Karua, Kaimu Waziri wa Mipango, Maendeleo ya Nchi na Dira ya 2030 Peter Kenneth, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Elimu James ole Kiyiapi, mbunge wa zamani Paul Muite, na mfanyabiashara Mohammed Abduba Dida -- walisimama mbele katika Shule ya Kimataifa ya Brookehouse huko Nairobi saa 1:30 usiku kwa saa za nchini na kujibu maswali kwa upana wa mada hadi saa 5 usiku. Mdahalo ulipangwa kuisha kwa masaa mawili.
Masuala yaliyozungumziwa wakati wa mdahalo yalikuwa ni
pamoja na utawala, usalama wa huduma za kijamii na siasa za vyama. Wagombea wote waliahidi kupambana na rushwa na ukabila, na walionekana kukubali kwamba utekelezaji wa katiba utakuwa ndiyo msingi wa kushughulikia masuala yote.
Ratiba ya mdahalo wa pili wa tarehe 25 Februari itakuwa ni kuhusu uchumi, ardhi, kukabidhi madaraka na sera ya kigeni.

Kesi ya ICC yavuta usikivu

Mdahalo wa Jumatatu ulivuta usikivu kwa kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) inayomhusisha mgombea urais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza William Ruto kwa tuhuma za kuhusika na utokeaji wa vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Kesi hiyo, ilipangwa kuanza tarehe 11 Aprili, inaweza kugongana na kampeni za uchaguzi, kutokea ndani ya mwezi kama mgombea huyo atashindwa kupata asilimia 51 ya kura katika awamu ya kwanza.
Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashitaka kwa tuhuma zao za kuhusika katika mauaji, ubakaji na vurugu zilizotokea baada ya kura za maoni mwaka 2007. Wote walikanusha kuhusika.
Alipoulizwa jinsi yeye na Ruto watakavyoweza kiuendesha nchi na kuhudhuria mahakamani kama wakichaguliwa, Kenyatta alisema, "Nitakuwa na uwezo wa kushughulikia suala hilo kusafisha majina yetu... wakati huo huo kuhakiksha kwamba kazi ya serikali inaendelea."
Lakini mkosoaji wake mkuu alihoji uwezekano wa kuiendesha Kenya akiwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyopo The Hague.
"Ninajua itaibua changamoto kubwa kuiendesha serikali kwa Skype kutoka The Hague," Odinga alisema. "Najua hilo haliwezekani."
Ingawa wakati mwingine aligusa mabadiliko -- kushindwa kwingi kwa Kenyatta kunatokana na kujiandaa kuhudhuria kesi ya msingi ya ICC -- aliyejibu alisisitiza umuhimu wa kutorudiwa kwa vurugu za kura za maoni za uchaguzi uliopita.
"Binafsi sina tofauti na mheshimiwa Raila... lakini tunaweza kutofautiana jinsi ya kushughulikia baadhi ya mambo," alisema Kenyatta, akimtazama Odinga.
Kujibu, Odinga alimuita Kenyatta "kaka yangu" na kusema walikuwa "marafiki wakubwa".

Kutenganisha siasa na ukabila

Wakenya walikusanyika katika vituo vya burudani na majumbani kuangalia mdahalo wa kihistoria, uliyoonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni, redio pamoja na kwenye intaneti kwa watazamaji wa nchi za nje.
Adams Oloo, mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye pia anaongoza idara ya sayansi ya siasa ya Chuo Kikuu cha Nairobi, aliiambia Sabahi mdahalo uliwapa wapigakura fursa ya kutathimini wagombea katika sera zao.
"Hii ni mara ya kwanza tunawaona wagombea urais wakieleza katika namna ya utulivu wana msimamo gani," alisema. "Wamekuwa wakitoa ilani zao kupitia mikusanyiko ya kisiasa katika kupitisha na tamthiliya nyingi na burudani ambavyo vimefanya iwe vigumu kwa umma hata kuwaelewa au kuwaamini."
Alan Mungai, mwenye umri wa miaka 30, msafisha viatu kutoka maeneo ya Langata karibu na Nairobi, alisema mdahalo ulimsaidia kuwatathmini wagombea kwa mara ya kwanza.
"Kwa mara ya kwanza, ilibidi niwapime kuhusu muktadha wa mambo mbalimbali, sasa ninaweza kufanya uchaguzi kwa kuwafahamu nikitenganisha kutokana na kabila," alisema. Baada ya kuangalia mdahalo Jumatatu usiku, Mungai, Mmeru, alisema aliamua kumpigia kura Kenyatta, ambaye anatoka kabila la Kikuyu.
Wanjiru Kimani, mwalimu katika Shule ya Msingi ya Karen C jijini Nairobi, alisema kuwaweka wagombea katika jukwaa moja kulisaidia kupunguza wasiwasi baina ya jamii za makabila mbalimbali.
"Wakionekana kukumbatiana, inaonyesha kila mmoja kuwa ndugu wakati na kabla ya mdahalo, ilikuwa vizuri kwa wafuasi wao kuona kwamba [wagombea] sio maadui --- wanatofautiana tu kwa mitazamo yao," alisema.
Hata hivyo wiki iliyopita, Wafuatiliaji wa Haki za Binadamu walihadharisha hatari ya vurugu za kisiasa nchini Kenya awali "zilikuwa kubwa", wakionyesha kwamba "sababu kuu ya vurugu zilizohusiana na uchaguzi uliopita zinaendelea kuwepo."

Vyombo vya habari vyaandaa tukio la kihistoria

Mkurugenzi wa uendeshaji wa midahalo Francis Munywoki alisema makadirio ya shilingi milioni 100 (Dola milioni 1.1) zilitumika katika mdahalo wa Jumatatu, zililipwa kwa ushirikiano wa vyombo vya habari vya Kenya ikiwa ni pamoja na Shirika la Habari la Taifa, Royal Media Services, Standard Group, Redio Africa, Shirika la Habari la Kenya, Media Max na vituo 34 vya redio.
"Hii ilikuwa ni fursa kwa wagombea kushirikisha watazamaji na kuwaonyesha hasa kinachowatofautisha wao dhidi ya wapinzani wao," Munywoki alisema kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation. "Hivi ndivyo tunavyotaka kutumia vyombo vya habari kusaidia wapiga kura kufanya uamuzi wakijua wakati wa uchaguzi na wakati huohuo kuleta amani."
Wakati mdahalo unakaribia kuanza baada ya wagombea wawili wanaojulikana kidogo -- Muite na Dida -- awali walikuwa wametengwa katika mkutano, kwa Muite kuwa na amri ya mahakama kuhakikisha kwamba wanaruhusiwa kuhusika, kwa mujibu wa AFP.