Mwanariadha mlemavu na bingwa wa mashindano ya Paralympics, Oscar Pistorius, anatarajiwa kurejea mahakamani mjini Pretoria hii leo kutoa maeleozo zaidi kuhusu kesi inayomkabili na kujua ikiwa atapewa dhamana.
Viongozi wa mashtaka wanapanga kumshtaki Oscar kwa kosa la mauaji , madai anayotarajiwa kuyapinga vikali.
Mwili wa marehemu Reeva unatarajiwa kuchomwa mjini Port Elizabeth.Mchumba wake aliyekuwa mwanamitindo, Reeva Steenkamp, alipigwa risasi nyumbani kwake siku ya Alhamisi. Polisi waliweza kupata bunduki katika eneo la
Bwana Pistorius aliwasili mahakamani kabla ya saa tatu asubuhi ambayo itakuwa mara ya kwenzi kesi hiyo inasikilizwa tangu alipozuiliwa na polisi na kulia mbele ya mahakama Ijumaa wiki jana.
Viongozi wa mashtaka wanatarajiwa kuwasilisha ushahidi wao dhidi ya Pistorius wakisema anyimwe dhamana kabbla ya kesi yake kuanza kusikilizwa.
Pistorius pia huenda akajitetea kwa mara ya kwanza tangu kesi yake kuwasilishwa mahakamani.
Mwanariadha huyo asiye na miguu yote alishikwa na polisi mwishoni mwa wiki na hajazungumza hadharani tangu mauaji hayo kufanyika.
Taarifa kutoka kwa familia ya Pistorius ilisema kuwa atakanusha madai yote yanayoandaliwa dhidi yake.
Wakati huohuo, familia ya marehemu imeelezea masikitiko yao kwenye jarida moja iliyochapishwa siku ya Jumatatu.
Mamake Marehemu alisema kile wanachotaka ni majibu tu, majibu ya kwa nini mauaji hayo yalifanyika kwa nini mwanao alifariki kwa njia hii.
Kesi ya Oscar kutaka kuomba dhamana haitapeperushwa hewani baada ya mawakili kukataa.
Aidha kesi inayomkabili Oscar imezua hisia kali nchini Afrika Kusini na kote duniani kwani mwanariadha huyo anasifika kama shujaa duniani kote.
Anasifika kama mwanariadha mlemavu aliyeshindana na wanariadha wasio walemavu katika michezo ya olimpiki mjini London.
HABARI NA BBC.