![]() |
Sep blatter - Raisi wa FIFA. |
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Bonifance Wambura alisema barua hiyo ya Fifa waliipata jana Jumatatu.
Wambura alisema kwamba Fifa wa
mebaini kupitia vyombo mbalimbali ya habari nchini kuwa Serikali kupitia waziri mwenye dhamana ya michezo ameonyesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF hasa baada ya kuamuru uchaguzi wa TFF ufanyike kabla ya Mei 25 mwaka huu.
"Kwa mujibu wa barua hiyo ya Fifa ya Machi 10, 2013 kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) akidai kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari
imeshafanyiwa marekebisho.
Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali huku ikidaiwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake, imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Fifa, Jerome Valke.
Barua hiyo ya Fifa imekuja ikiwa ni wiki moja tangu serikali iwatake TFF hadi kufikia jana Jumatatu (Machi 11) wawe imeshatoa tamko la kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na serikali ya kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba hadi ifikapo Aprili 15 pamoja na kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi ambao unatakiwa ufanyike kabla ya Mei 25.
Serikali pia imejikuta ikiingia kwenye mgogoro na TFF baada ya kuikataa katiba yao kwa vile ilikiuka taratibu kwa kufanya marekebisho yake kwa njia ya waraka badala ya kuitisha mkutano mkuu kitu ambacho kilipingwa na TFF kwa madai kuwa waliamua kufanya vile kwa kuwa hawakuwa na fedha za kuitisha mkutano na kuitaka serikali kutowaingilia kwa vile TFF ni chama kamili na kina uhuru wake kamili kama vilivyo vyama vingine.
Kwa mujibu wa Wambura, alisema Fifa imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.
Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa Fifa wanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya Fifa inayokataza serikali kuingilia masuala ya wanachama wake,'' ilieleza barua hiyo ya Fifa ambayo nakala yake imepelekwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Awali uchaguzi mkuu wa TFF ulipangwa kufanyika Februari 24 lakini uliingia doa baada ya serikali kuifuta katiba ya mwaka 2012 iliyotumika kuitisha uchaguzi huo huku baadhi ya wagombea wakienguliwa katika kinyang'anyiro hicho.