Licha ya kuifunga Bayern Munich ya Ujerumani mabao
mawili kwa bila ugenini, Arsenal waondolewa katika mashindano ya Klabu
bingwa bara Ulaya.
Hii ni kwa sababu katika mechi ya awali
iliyochezwa wiki mbili zilizopita katika Uwanja wa Emirates, Arsenal
walifungwa magoli 3-1 na Bayern.Kufuatia bao hilo Arsenal wakawa wanahitaji magolo mengine mawili ili kumaliza mechi wakuwa juu kwa 3-0.
Mlinda lango wa
Arsenal Lukasz Fabianski alifanya kazi ya ziada kwani alipangua mikwaju kadhaa kutoka kwa mshambulizi matata Arjen Robben hivyo kumnyima nafasi ya kuifungia Bayern Munich goli lolote.
Lakini baada ya mechi , Bayern Munich ndio walifaulu kuingia hatua ya robo fainali.