Habari zaidi, viongozi wa kutoka mataifa ya Latin
Amerika, wamekuwa wakituma pongezi zao kwa Papa mpya mteule wa kanisa
Katoliki
Francis 1. Papa huyo anatokea nchi ya Argentina, na anakuwa
Papa wa kwanza kutoka sehemu hiyo.
Argentina, ikiwa ndio asili ya Papa, ilikuwa na
sababu kubwa zaidi kusherehekea uteuzi wake. Licha ya uhusiano wa
msuguano kati ya rais wa Argentina, Christina Fernandez, alikuwa wa
kwanza kutuma pongezi kwa Papa Francis, h
uku akimtakia kila kheri katika
kupigania haki na usawa.
Wawili hao waliwahi kutofautiana hadharani juu ya suala la ndoa ya watu wa jinsia moja.
Rais wa Brasil Dilma Rousef atuma pongezi kwa Papa
Nchini Brasil, inayotazamiwa kuwa na idadi kubwa
zaidi ya waumini wa kanisa hilo la Roma duniani, rais Dilma Rousef
alimpongeza sana Papa Francis, na kwa jumla wananchi wa Argentina. Pia
alimkaribisha Papa Francis kwa moyo mkunjufu kuhudhuria sherehe za
kuadhimisha siku ya vijana duniani mnamo Julai, mjini Rio.
Kwa rais wa Chile, Sebastian Pinera alisema kuwa
ameridhishwa na kuwa Papa huyo mpya anaielewa nchi ya Chile vizuri sana
na hata akamkaribisha kuja kuzuru tena.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, yeye
alifurahishwa zaidi na kuwa kwa Mara ya Kwanza wamepata Papa ambaye
lugha yake ya mama ni Kispania.