Real Madrid imefuzu kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa wachezaji 10 Manchester United mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Real ilipata mabao yake kupitia kwa Luka Modric na Cristiano Ronaldo na kufuta makosa ya Sergio Ramos aliyejifunga mwenyewe kwenye mchezo huo, ambapo Luis Nani alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Nahodha wa Real Madrid, Ramos alijifunga mwenyewe katika dakika 48, wakati akijaribu kuzuia krosi ya Nani na kumpoteza kipa wake Lopez kabla ya kujaa wavuni.
Manchester United
walipata pigo katika dakika 57, baada ya kiungo wake Nani kuonyesha kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya beki wa Real, Arbeloa.
Kitendo cha kutoka mchezaji Nani na kuingia Luka Modric kuliirudisha Real mchezoni na katika dakika 66 walisawazisha bao hilo kwa shuti kali la Modric kabla ya Ronaldo kuipa Real bao la ushindi dakika 69 akimalizia vizuri krosi ya kutoka kwa Higuain.
Ronaldo baada ya kufunga bao lake 118 katika michezo 292 aliyoicheza Real hakushangilia kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Manchester United waliamka na kuanzisha mashambulizi mengi golini kwa Real, lakini kipa wa Lopez alikuwa kikwazo kikubwa kwao.
Katika mchezo mwingine uliofanyika Uwanja wa BVB, wenyeji Borussia Dortmund waliutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kushinda magoli 3-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa Juventus kuivaa