![]() |
Michael owen |
mkataba maalumu.
MICHAEL Alianzia wapi?
Michael Owen amesema anashukuru kuona taaluma yangu ya mpira wa miguu imenifikisha sehemu ambapo nilikuwa nikiota kupafikia.
Alianza kuwika akiwa na kikosi cha
Liverpool na dunia ilimtambua zaidi kwenye miaka ya 1998 akiwa na umri wa miaka 18 wakati alipoitwa kwenye kikosi cha England kilichoshiriki kombe la Dunia mwaka huo na bao lake la pekee dhidi ya Argentina kwenye michuano hiyo lilimpa umaarufu zaidi kabla ya kufunga mabao matatu peke yake maarufu kama hat trick katika mechi ambayo England iliwafunga Ujerumani kwa mabao 5-1 mwezi Septemba mwaka 2001.
Hadi hivi sasa Owen amekwisha funga jumla ya magoli 220 kwenye klabu alizochezea,Huku akitwaa Mataji ya Ligi kuu soka nchini England,Kombe la FA,Kombe la Ligi mara tatu na kombe la Uefa.
Mwaka 2001,Owen alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya,akiwa ni Muingereza wa kwanza kutwaa tuzo hiyo baada ya Kevin Keegan aliyetwaa kwenye miaka ya 1976.
Mwaka 2005,Owen alipata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu wake akiwa anaichezea timu yake ya taifa,Toka hapo amekuwa ni mwenye kusumbuliwa na majereha ya mara kwa mara.
Toka amejiunga na timu yake ya sasa ya Stoke City,Owen amekwisha funga bao moja tu katika michezo saba aliyoichezea timu hiyo.
Michael Owen,amezishukuru klabu zake zote alizowahi kuchezea pamoja na mashabiki wake toka akiwa Liverpool mpaka sasa Stoke ambapo amesema kwa sasa hana tena miaka 18 na hana budi kuachana na soka la ushindani,aliandika katika mtandao wake.
Pamoja na yote,Owen atandelea kukumbukwa na waingereza wote kutokana na kipaji chake pamoja na bao lake pekee na la muhimu katika michuano ya kombe la dunia dhidi ya Argentina.