"Mashambulizi ya kujitoa muhanga yalifanyika karibu na Jengo la Maonyesho la Taifa kwenye wilaya ya Hamarweyne ya
mji mkuu pale gari iliyobeba mabomu ilipolivamia basi la abiria," taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia, Abdi Farah Shirdon, ilisema. "Kiasi cha watu 10 waliuawa na 15 kujeruhiwa."
mji mkuu pale gari iliyobeba mabomu ilipolivamia basi la abiria," taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia, Abdi Farah Shirdon, ilisema. "Kiasi cha watu 10 waliuawa na 15 kujeruhiwa."
Waasi wa al-Shabaab wenye mafungamano na al-Qaida baadaye walidai kuhusika na mashambulizi hayo na kumtaja afisa wa ujasusi aliyelengwa.
"Mujahidina walihusika na mashambulizi haya dhidi ya kafiri Khalif Ereg," msemaji wa al-Shabaab, Sheikh Ali Mohamud Rage, aliliambia shirika la habari la AFP, akimaanisha Mkuu wa Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa wa mkoa wa Benadir, Kanali Khalif Ahmed Ereg.
"Mashambulizi dhidi ya watu aina yake yataendelea hadi waangamizwe kabisa kutoka ardhi tukufu ya Somalia," alionya Rage.
Hata hivyo, Shirdon alisema kwamba mashambulizi hayo yalikuwa "majaribio yaliyoelekezwa kutuvunja moyo ambayo haytakua na athari yoyote."
"Tumeshapiga hatua nyingi sana mbele kuweza kurudi kwenye siku mbaya za kale," alisema. "Amani, utulivu na biashara ndio hali ya leo."
"Haya yalikuwa mashambulizi ya kioga dhidi ya Wasomali wasio na hatia yaliyolengwa kuzirudisha nyuma jitihada za watu wa Somalia kujiondoa kwenye miaka kadhaa ya kutokuwa na utawala wa sheria," alisema Luteni Jenerali Andrew Gutti wa Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kupitia Twitter.
"Mashambulizi ya leo hayakubaliki kabisa," alisema Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Augustine Mahiga. "Somalia imepiga hatua kubwa kuelekea kwenye njia ya maendeleo na utulivu na mashambulizi haya ya kijoga ya kigaidi yataongeza tu uthubutu wa watu wa Somalia kusonga mbele."