London, England. KochaArsene Wenger amesema haoni
shida kuwaambia wachezaji wake kujipanga na kuwapongeza wenzao wa
Manchester United kwa kutwaa taji la Ligi Kuu England, lakini amepania
kuhakikisha mabingwa hao wapya wanaondoka Uwanja wa Emirates
wakiinamisha vichwa chini.
United inakwenda kwenye dimba la Emirates leo
katika mchezo wa Ligi Kuu, huku mshambuliaji Robin Van Persie akirejea
kwenye uwanja wake wa zamani alikokuwa nahodha kabla ya kujiunga na
United.
United inataka kutumia mechi hiyo kama sehemu ya
kunogesha sherehe ya kutwaa taji la 20 England, lakini hilo likiwezekana kwa kuifunga Arsenal iliyojizatiti kuitubulia United.
kunogesha sherehe ya kutwaa taji la 20 England, lakini hilo likiwezekana kwa kuifunga Arsenal iliyojizatiti kuitubulia United.
Ingawa macho yatakuwa zaidi kwa Robin, sehemu nyingine ya mchezo huo inatarajiwa kujaza ushindani mkubwa.
United iliivua ubingwa Manchester City, na kwenye
mchezo wao dhidi ya Arsenal hawana cha kupoteza zaidi ya kulinda heshima
na kutaka kuweka rekodi.
Tofauti kwa Arsenal, ushindi kwao ni lazima ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania nafasi nne za juu kwenye msimamo.
City imejiimarisha vizuri kwenye nafasi ya pili na
kazi kubwa iko kwa Arsenal inayowania kumaliza katika nafasi ya tatu,
sambamba na Chelsea watakaocheza na Swansea kwenye uwanja wao wa
nyumbani leo na Tottenham wanaoshika nafasi ya tatu, ambao jana walikuwa
dimbani kucheza na Wigan.
Arsenal wako pointi moja mbele ya Chelsea na mbili mbele ya Tottenham na wanatarajia kujiimarisha zaidi kwa kuifunga United.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamechukizwa na
uamuzi wa Wenger kuwaruhusu wachezaji wake kuwapa heshima United kwa
kutwaa taji kabla ya mchezo wa leo, ikiwa ni marejeo kama hayo
yaliyofanywa na wachezaji wa kikosi cha Alex Ferguson kilichowapa
heshima Gunners walipotwaa ubingwa mwaka 1991.
Mashabiki hao wa Arsenal walisema kama uamuzi wa
kocha Wenger utabaki kama ulivyo, basi watageuza migongo yao uwanjani
wakati wachezaji wa United watakapopewa heshima.