Arusha. Marais watano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, wanakutana jijini hapa katika mkutano wa dharura, ambapo pamoja na mambo mengine watajadili itifaki ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini Novemba mwaka huu.
Marais hao ni Yoweri Kaguta Museveni Rais wa
Uganda, ambaye ndiye Mwenyekiti, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Pierre
Nkuruzinza wa Burundi, Paul Kagame wa Rwanda na Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta, wote walitarajiwa kuanza kuwasili jana Arusha.
Kenyatta anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa leo,
kwani atakuwa anahudhuria kwa mara ya kwanza katika vikao vya EAC jijini
Arusha kama Rais wa Kenya.
Katika kikao cha marais hao,
ambacho kitafanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, pia anatarajiwa kuapishwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki anayetokea Kenya, Charles Njoroge na pia kuapishwa majaji wawili wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki, Dk Faustin Ntezilyayo kutoka Rwanda na Liboire Nkuruzinza kutoka Burundi.
ambacho kitafanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, pia anatarajiwa kuapishwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki anayetokea Kenya, Charles Njoroge na pia kuapishwa majaji wawili wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki, Dk Faustin Ntezilyayo kutoka Rwanda na Liboire Nkuruzinza kutoka Burundi.
Kikao cha marais hao, kilitanguliwa ni kikao cha
makatibu wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na pia Baraza la
Mawaziri wa Jumuiya hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari ya Katibu
mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Dk Richard Sezibera, alisema mawaziri wa jumuiya hiyo, pia
walijadili itifaki wa umoja wa fedha kwa nchi hizo na taarifa yao
itapelekwa kwa marais leo.
Pia mawaziri hao, walijadili bajeti ya jumuiya
hiyo ya mwaka 2013/14 ya Dola 117,238,966, walijadili pendekezo la
kuongezea wigo na mamlaka Mahakama ya Afrika ya Mashariki na pia
uandaaji wa itifaki ya haki na kinga kwa watumishi wa jumuiya ya Afrika
ya mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa
Afrika ya Mashariki wa Tanzania, Samweli Sitta alisema tayari baraza la
mawaziri, limepitisha bajeti ya jumuiya hiyo na taasisi zake zote.
Sitta alisema kuhusiana nauuamuzi wa masuala
mbalimbali ambayo yalijadiliwa na mawaziri hao, taarifa rasmi itatolewa
leo na marais baada ya kuyapitia .
Hata hivyo, alisema katika kikao cha mawaziri,
Kenya iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya kwa kuwa bado Waziri wa
Kenya hajathibitishwa na bunge.