Thursday, May 2

Barcelona chali: yachabangwa 3-0 na Bayen Munich klabu bingwa ulaya.


Kwa mara ya kwanza, fainali ya michuano hiyo sasa itazikutanisha timu zote kutoka Ujerumani, baada ya Dortmund kuiondoa kwenye mashindano Real Madrid
Bayern Munich ya Ujerumani imeitia aibu Barcelona ya Hispania kwa kuiangushia kipigo kinene cha mabao 3-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani, na hivyo kukata tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-0.
Fainali ya michuano hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Wembley, England Mei 25 mwaka huu.
Katika mchezo wa
kwanza uliofanyika Ujerumani, Bayern moja ya timu bora Ulaya kwa sasa, waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 na kuhitaji angalau sare ili kusonga mbele.
Kichapo hicho kinaweka historia ya vipigo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini pia ni cha kwanza na pekee kwa aina yake kupata Barcelona katika mashindano hayo ya klabu Ulaya.
Kwa mara ya kwanza, fainali ya michuano hiyo sasa itazikutanisha timu zote kutoka Ujerumani, baada ya Dortmund kuiondoa kwenye mashindano Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-3 katika nusu fainali ya kwanza.
Barcelona haikuonekana kama ilikuwa na dhamira ya kufuta kipigo cha mabao 4-0 walichopata katika mchezo wa kwanza, huku pengo la kinara wa mabao Lionel Messi aliyeshuhudia mchezo huo akiwa jukwaani likionekana wazi.
Kipigo hicho kimeshindwa kurejesha historia ya michuano ya klabu Ulaya kama ilivyowahi kufanywa na Partizan Belgrade,Real Madridtimu na Leixosa katika misimu tofauti.
Arjen Robben akifunga goli la kwanza.

Partizan Belgrade walisonga mbele baada ya kufaidika na bao la ugenini na kufanya matokeo kuwa 6-6 kufuatia mchezo wa awali kufungwa 6-2 katika michuano ya Kombe la Uefa msimu wa mwaka 1984-85.
Real Madrid walinyukwa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza raundi ya tatu Kombe la Uefa dhidi ya Borussia Moenchengladbach msimu wa mwaka 1985-86, lakini waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano.
Timu ya Lexios ya Ureno katika msimu wa mwaka 1960-61 wakati wakishiriki michuano ya Kombe la Washindi Ulaya, walichapwa 6-2 na timu ya Chaux kutoka Uswisi, lakini walisonga mbele kwa ushindi wa mabao 5-0 katika mechi ya marudiano.
Kiungo Arjen Robben alifunga bao la kwanza kwa Bayern muda mfupi baada ya mapumziko alipopenya ndani ya boksi la hatari na kupiga shuti lilikowenda moja kwa moja kwenye nyavu za juu za lango la  Barcelona dakika ya 48.