Thursday, May 2

Chelsea ileee; yatinga fainali ya europa, yaifunga Fc Basel 3-1.

Beki wa Chelsea aliye katika kiwango chake cha juu David Luiz alisema upande wao wana njaa ya kupata mafanikio katika Ligi ya Europa baada ya ushindi wao wa 3-1 wa nusu fainali dhidi ya Fc Basel ya Uswis.
Luiz alifunga katika mechi zote nne za mwisho nyumbani na ugenini akiwafunga mabingwa wa Uswisi, na pia alifunga katika shambulizi la kwanza jijini London dhidi ya Fulham  Aprili na - kufanya afunge mabao matatu katika michezo mitano iliyopita kwa vijana wa Rafael Benitez.

Watakutana na viongozi wa Liga Benfica timu ambayo Luiz aliicheze kabla ya kujiunga na Chelsea  mwaka 2011.
Mlinzi huyo wa Brazil alisema kulikuwa hakuna uhaba wa motisha kwa ajili ya Mabingwa msimu uliopita wa Ligi ya washindi kupata mafanikio zaidi juu ya hatua ya Ulaya.

"Tuna fainali moja zaidi ya kushinda kwa sababu nataka taji moja zaidi," alisema baada ya
ushindi katika mchezo huo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge siku ya Alhamisi.

 "Mimi si tu kwamba nataka kufika fainali ... utakuwa mchezo mgumu dhidi ya klabu kubwa, timu nzuri hivyo tunahitaji kushinda mechi hiyo.




 
"Bila shaka Benfica ni timu ambayo kila mtu anaijua, ni timu ambayo ipo katika moyo wangu kwa sababu wao walinipa nafasi ya kuja Ulaya na kuonyesha kipaji changu cha soka.

"Hata hivyo, wakati tutakapoanza mchezo huo, mimi nitasahau kwakuwa na mimi nataka kushinda na mwisho wa mchezo tuwe washindi." 



Luiz aliusifia ushawishi wa kocha wa mpito wa Chelsea Benitez, akidai Mhispania huyo huwashirikisha mengi ya hekima kwaajili ya kuboresha viwango vyao.

"Nadhani Rafa amefanya kazi kwa bidii pamoja nami na wachezaji wote mmoja mmoja hivyo mimi humsikiliza sana," Luiz alisema.

"Yeye ni mkubwa kuliko mimi na hivyo unahitaji kumsikiliza Yeye ana uzoefu zaidi kuliko mimi na ana mtaji zaidi yangu na unahitaji kujifunza kutoka kwake.


 "Yeye anajaribu kunifundisha vitu kuhusu mambo ya soka ya kila siku na mimi hupenda kujifunza mambo haya.
"Yeye amenisaidia  mengi msimu huu, kila mtu anaweza kuona uwanjani na kila siku mimi husema asante kwa sababu yeye ni kocha wa ajabu."