Wednesday, May 8

Mkutano wa London kuhusu Somalia wafunguliwa, wasisitiza ushirikiano wa usalama

Mkutano wa Kimataifa wa kuongeza utulivu wa kisiasa nchini Somalia ulifunguliwa huko London Jumanne (tarehe 7 Mei), kwa kuandaliwa kwa pamoja na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.
Katika kufungua mkutano huo, Cameron alipongeza kuboreka kwa usalama wa Somalia katika miezi ya hivi karibuni, lakini alitahadharisha kushindwa kusaidia ujenzi mpya wa Somalia kutasababisha "ugaidi na uhamiaji wa wengi".
"Changamoto hizi sio tu masuala ya Somalia. Yana maana kubwa kwa Uingereza -- na jumuiya yote ya kimataifa," alisema. "Kwa nini? Kwa sababu mawo yenu yakiharibiwa na misimamo mikali na kuelekea katika ugaidi na kuwa na misimamo mikali, usalama wa ulimwengu mzima utakuwa hatarini."
Wawakilishi wa zaidi ya nchi 50 na mashirika wamehudhuria mkutano huo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Shirika la Fedha Duniani.
Mohamud alisema nchi imewakaidi walio na mashaka tangu mkutano wa awali huko London mwaka jana na kuwa "mengi yalifikiwa kuliko ambavyo ilitegemewa".
Alionya, hata hivyo, mengi yanatakiwa kufanyika.
"Watu wanaweza kuuliza kwa nini Somalia ni muhimu safari hii lakini kuna kubwa iliyo muhimu sasa hivi: siku zijazo za nchi, usalama wa mkoa na dunia nzima, na uondoaji wa ngome za maharamia katika Ghuba ya Aden," alisema. "Tunahitaji msaada; tunahitaji usaidizi na uwekezaji; na tunahitaji ulinzi dhidi ya wote wanaojaribu kutushambulia."
Umoja wa nchi za Ulaya umeahidi euro milioni 44 (dola milioni 58) kuisaidia Somalia, nusu yake itatumika kutoa mafunzo na kuwaandaa maofisa polisi wa Somalia, mahakimu na viongozi wengine.
"Nchini Somalia, kama mahali pengine popote, kunaweza kuwa hakuna maendeleo bila usalama," Kamishna wa Maendeleo wa EU Andris Piebalgs alisema katika taarifa. "Tunatoa msaada huu mpya kuonyesha kwa mara nyingine Uwajibikaji wa Umoja wa Ulaya katika kusaidia watu wa Somalia kuunga mkono utawala bora, usalama, haki na polisi."