Bajeti ndogo inayotolewa na Serikali katika vituo vya afya nchini ni chanzo cha ongezeko la vifo vya Malaria nchini.Kutokana na hali hiyo ya kutolewa bajeti ndogo kwa Serikali inasababisha ukosefu wa vifaa vinavyohitajika katika vituo vya afya katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria.
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Malaria na Magonjwa ya watoto chini ya miaka mitano Dk. Zena Mtajuka.
Mtajuka alisema bajeti inayotolewa na serikali ya kukabiliana na kudhibiti ugonjwa huo ni finyu sana haiwezi kukabiliana na kumaliza tatizo hilo.
Alisema kuwa bajeti hiyo inasababisha kukosekana kwa vifaa na vipimo madhubuti katika vituo vya afya na kupelekea vifo vinavyotokana na malaria vya watoto chini ya miaka mitano kuongezeka siku hadi siku.
Hivyo alitoa wito kwa serikali kutoa bajeti kubwa ya kutosheleza kwenye vituo vya afya ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
NIFAHAMISHE.