Friday, July 5

Azaliwa na Ugonjwa wa Ajabu Aona Dunia Chini Juu

Mwanamke mmoja nchini Serbian, anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu unaomfanya kuona Dunia na vilivyomo ndani yake chini juu, amekuwa akisumbuliwa na hali hiyo iliyosababishwa na matatizo kwenye ubongo wake.
Bojana Danilovic (28) alizaliwa akiwa na hali nadra kumtokea mtu, hali ambayo imemfanya awe anaona kila kitu kilichopo mbele yake kipo chini juu, ugonjwa huo unaofahamika kitaalamu kwa jina la spatial orientation hugeuza mfumo wa ubongo na kumfanya mtu aone kila kitu kipo chini juu.

Wanasema macho yangu yanaona picha katika njia sahihi, lakini ubongo wangu huibadilisha, alisema Danilovic.

Kama utabahatika kuona dawati la Danilovic, unaweza kuzani huwenda anafanya utani, Keyboard ya Computer yake, Monitor na Karatasi anazozichapisha vyote huvigeuza chini juu.

Pamoja na changamoto zote hizo zinazomkabili, lakini amefanikiwa kumaliza masomo yake ya chuo kikuu katika Kitivo cha Uchumi na kupata alama za juu.


NIFAHAMISHE.