Maana ya kompyuta ( tarakirishi ).ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea
na kukusanya taarifa (Data), kufanyia kazi na kutoa matokea ya kazi hiyo
na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu
kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information)kwa haraka .
Tarakilishi ( computer. ).ni mashine inayotumia data kwa njia tofauti kutokana na maagizo zilizoandikwa kwenye bidhaa pepe (kwa Kiingereza software).
Maneno Kompyuta na Ngamizi yanaweza kutumika badala Tarakishi.
Teknolojia hii ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia
ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa
huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli
mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.
Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu.
HATUA KABLA YA MWANZO WA KOMPYUTA (1642).Msomi mmoja kutoka Ufaransa aliyekuwa anaitwa Pascal, alianzisha chombo
cha kufanyia hesabu, ambacho alikitengeneza kwa ajili ya kumsaidia baba
yake katika kazi za hesabu, lakini hakikuwa na sifa bora kama
ilivyotakiwa. Kisha baada ya hapo kiliendelezwa na msomi mwengine kutoka
Ujerumani, ambaye alijulikana kwa jina la Lebnitz na kuzidishwa ubora
zaidi, kikawa kinafanya kazi zote za hesabu, kama vile kujumlisha,
kutoa, kugawanya na kuzidisha, badala ya kufanya kazi za kuzidisha na
kugawanya tu. Kisha msomi mwengine kutoka Uingereza alikuja kuanzisha
chombo chengine cha hesabu, ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa
kuhifadhi vitu. Chombo hicho kilikuwa na sehemu kuu tatu, ambazo sehemu
ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu, sehemu ya pili
ilikuwa ni kwa ajili ya kufanyia hesabu, na sehemu ya tatu na ya mwisho
ilikuwa ni kwa ajili ya kuchapishia.
HATUA YA MWANZO (1944.)Kipindi cha mwaka 1944 kinajulikana kuwa ni mwanzo wa kudhihiri
kompyuta. Kompyuta katika kipindi hicho ilikuwa ina sura tofauti na hivi
sasa, kwani ilikuwa ni kubwa mfano wa chumba, na ilikuwa inatumika kwa
ajili ya kufanyia hesabu tu, na ilikuwa inajulikana kwa jina la (ENIAC)
Electronic Numerical and Calculation. Na mwisho wa mwaka 1951
ilianzishwa kompyuta nyingine ambayo ilikuwa inaitwa Unifac, na
ilitengenezwa kwa ajili ya kufanyia biashara, na ilikuwa ni chombo pekee
ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu.
HATUA YA PILI (1958).
Kipindi cha mwaka 1958 kilifanikiwa kuendeleza chombo cha kompyuta,
ambapo kilianzishwa chombo kinachoitwa Transistor, ambacho kiliwezesha
kutengeneza kompyuta yenye umbo dogo baada ya kuwa na umbo kubwa mfano
wa chumba. Vile vile chombo cha Transistor kiliwasaidia watumiaji wa
kompyuta kipindi hicho kuepukana na joto kali lililokuwa linatoka kwenye
kompyuta hiyo na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Na mwanzo wa miaka ya
sitini shirika la IBM lilianzisha chombo chengine cha kompyuta ambacho
kilikuwa na maendeleo zaidi katika kipindi hicho.
HATUA YA TATU (1964).Kipindi hichi kilileta maendeleo makubwa sana katika kompyuta, ambapo
chombo cha kompyuta kilitengenezwa kwa kutumia (Integrated Circuits)
chombo hicho kilichukua nafasi ya Transistor. Na pamoja na maendeleo
makubwa kutokea mwaka 1972 shirika la Intel lilifanikiwa kutengeneza
Processor ndogo ambayo ilibadilisha sura nzima ya kompyuta katika umbo
dogo sana (Mini Computer). Na hiyo ilikuwa ni sifa pekee ya mabadiliko
makubwa ya kompyuta, na katika kipindi cha mwaka 1975 shirika la IBM
lilianzisha kompyuta ya kutumiya mtu mmoja (Personal Computer), vile
vile katika kipindi hicho zilianzishwa programu za kuendeshea vifaa vya
kompyuta, na miongoni mwa programu hizo ilikuwepo programu ya (Dos) Disk
Operating System, Application Programs, na programu za kutengeneza
picha (Graphics).
HATUA YA NNE (1982).Mwanzoni mwa miaka ya themanini kulianza kuenea matumizi ya kumputa
zenye kutumia Hard disk, na Processor zenye umbo dogo (Micro Processors)
pamoja na programu za kuendeshea kompyuta (Operating System). Pia
zilianzishwa kopi za programu za kuendeshea kompyuta (Dos), na hapo
ndipo ilikuwa mwanzo wa kutumia windozi (Windows), na pia zilitumika
programu nyingine ndani ya Windozi kama vile Word, Word 2, Word 6, Excel
na power Point.
HATUA BAADA YA HATUA YA NNE. Kitu kinachosifika sana katika kipindi hichi ni kudhihiri kwa programu
za Windozi na kuwa kama ni mazingira pekee ya kuendeshea kompyuta, na
inajulikana wazi kwamba windozi ni kiini cha uendeshaji katika kazi za
kompyuta, na imeitwa windozi kwa sababu unaweza kuitumia kufanyia kazi
nyingi kwa wakati mmoja kwenye madilisha tofauti, kwa mfano pale
mtumiaji anapokuwa anasubiri windozi moja ifunguke anaweza kuwa anasoma
au kufanya kazi nyingine kwenye windozi nyingine pia.. Na windozi ya
kwanza kudhihiri ilikuwa ni Windows 95, 98, 2000, Millennium kisha
Windows XP, vili vile zilianzishwa programu maalumu kutoka kwenye
shirika la Microsoft, kama vile Microsoft Office 97, Microsoft Office
2000 na Microsoft Office 2003, ambazo ambazo zinakusanya ndani yake
Microsoft Word, Excel, Access na Power Point, pia zinajulikana kwa jina
la application programs. Kisha kiliendelezwa kifaa cha Processor kutoka
Pentium kwenda Pentium 2, Pentium 3 na Pentium 4, pamoja na kuzidi
uwepesi wa kufikia vitu mpaka Giga Byte 2. Pia ilizidishwa nafasi ya
kuhifadhia data ndani ya Hard disk kiasi cha kufikia Giga Byte 300, na
kufikia nafasi ya Ram zaidi ya Mega Byte 512.