Kompyuta imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
I. Sehemu zinazoshikika (Hardware)Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu.
Vifaa vya kuingizia vitu (Input devices):
- kibodi (keyboard)
- Mausi (Mouse)
- Skana (Scanner)
- Makrofoni (Microphone)
- Kamera (Camera)
Kibodi inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi Function keys).
JEDWALI LINALOONYESHA FUNGUO NA KAZI ZAKE:
Jina la funguo Kazi yake Home Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwanzo wa mstari End Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwisho wa mstari.
Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari.
Inatumika kwa ajili ya kuhamia upande wa kushoto mwa mstari.
Inatumika kwa ajili ya kuhamia upande wa kulia mwa mstari.
Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari. Pg Up Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari. Pg Dn Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari. Num lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia namba na michoro. Caps lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia. Enter Inatumika kwa ajili ya kutekeleza amri, au kuanzisha fungu la maneno kwenye ukurasa.. Del “Delete” Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya mbele yake.
“Back space" Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya nyuma yake. Space “Space bar” Inatumika kwa ajili ya kuweka masafa kati ya maneno. Esc “Escape” Inatumika kwa ajili ya kuacha kutekeleza amri. Tab Inatumika kwa ajili ya kuwacha masafa maalumu tofauti na ya kawaida (Normal).
Ctrl “Control” inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Alt inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Shift inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu. Alt-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia lugha. Ctrl-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia mwelekeo ndani ya ukurasa (kulia au kushoto) Print screen Inatumika kwa ajili ya kupiga picha kitu chochote kwenye kompyuta.
Ctrl-Alt-Del Inatumika kwa ajili ya kuwasha upya kompyuta.
3. MAUSI (MOUSE):
Kuna vitufe viwili kwenye kila mausi, kitufe cha upande wa kushoto (Left click) kinatumika kufungulia windozi, programu na kuchagulia maandishi, maneno na picha, na kitufe cha upande wa kulia (Right click) kinatumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kazi.
4. SKANA (SCANNER)
Skana inatumika kwa ajili ya kuingizia picha ndani ya kompyuta. Na kitu chochote kile kinachoingia ndani ya kompyuta kwa njia ya skana kinapewa sifa ya picha.
5. MAKROFONI (MICROPHONE):
Makrofoni inatumika kwa ajili ya kuingizia sauti ndani ya kompyuta.
6. KAMERA (CAMERA):
Kamera inatumika kwa ajili ya kupigia picha na kuingiza ndani ya kompyuta.
Viafaa vya kutolea vitu (Output devices):
1. SKRINI (SCREEN):
Skrini inatumika kwa ajili ya kuonyeshea matokeo ya vitu vilivyofanyika ndani ya kompyuta.
2. KIPAZA SAUTI (SPEAKER):
Kipaza sauti kinatumika kwa ajili ya kutolea sauti kutoka ndani ya kompyuta.
3. PRINTA (PRNTER):
Printa inatumika kwa ajili ya kutolea vitu vya maandishi au picha kwenye kompyuta kwa njia ya karatasi (kuchapisha).
4. PLOTA (PLOTER):
Plota ni ni chombo kinachotumika kwa ajili ya kutolea vitu, ambacho kinafanana na printa katika ufanisi wake wa kazi, lakini umbile lake ni kubwa kuliko printa, na kinatumika kwa ajili ya kuchapishia picha na michoro ya kiufundi, pia kinaweza kutumika kwa ajili ya kuchapisha maandishi kama herufi namba na alama.
II. Sehemu zisizoshikika (Software):
Kompyuta haiwezi kufanya kazi mpaka kipatikane kitu kinachoitwa software, ambocho kinawakilisha programu zinazoendesha kompyuta. Na programu hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
1. Programu za kuendeshea kompyuta (operating systems), programu hizo zinaitwa windows, na kuna aina nyingi za windows kulingana na toleo lake na ubora wake, kwani kila siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo tunapozidi kupokea programu nyingine za windows na zenye ubora zaidi kuliko zile zamani.
2. Programu za kufanyia kazi (application systems), nazo ni Microsoft Office na Graphics design, programu hizo daima zinafanya kazi ndani ya windows, ambazo zinatumika kwa ajili ya kazi mbali mbali za uandishi na hesabu, na kazi nyenginezo za kuunda na kutengeneza picha n.k.
vifaa vya kuendeshea vifaa vya kuingizia na kutolea vitu:
Vifaa hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho (C.P.U) kifupi cha Central Processing Unit, ambacho ni kiini cha kompyuta na ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vyote vya kompyuta na kutoa maelekezo yote. Na C.P.U. ni sehemu kuu ya nguvu ya kompyuta, au kitovu cha kompyuta.
Kazi za C.P.U:
1. Kutawala (Control): Ndani ya madhabodi (Motherboard) kinapatikana kifaa kinachoitwa (Bios) kifupi cha Basic Input Output System, ambacho ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vya kuingizia na kutolea vitu. Na ni vigumu kufuta au kurekebisha vitu vilivyomo ndani ya kifaa hicho kwani vinazingatiwa ni vitu vya kusomea tu na si kwa kazi nyingine.
2. akili na mahesabu (arithmetic logical):
Kazi za mahesabu ni kazi zote zinazofanyika na hesabu, kama vile kutoa, Kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Na za akili
WINDOWS XP:
Windows Xp inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa Windows za kisasa zenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zile za zamani, kama Windows 95, Windows 98 na Windows Millenium.
SIFA ZA WINDOWS XP:
- Uwepesi wa kuanza na kumaliza kutumia.
- Uwezo wa kutumia lugha mbili mfano kingereza na kiarabu, pia uwezo wa kubadilisha lugha hizo na kuweka nyengine.
- Kufungua kurasa kwa haraka.
- Uwezo wa kuendesha programu zaidi ya moja katika wakati mmoja.(Multitasking)
- Uwezo wa kuhifadhi vitufe (files) vilivyofutwa katika recycle bin.
- Uwezo wa kufanya kazi katika mdahalishi (Network) kwa haraka.
- Uwezo wa kubadilishana vitu (Data) kati ya programu tofauti.
- Kutumia majina marefu zaidi ya herufi 255 katika jina la faili moja.
- Haraka na uwepesi katika utekelezaji.
- Vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya kazi katika net.
- Uwezo wa kutambua idadi nyingi ya vyombo vilivyounganishwa ndani ya kumpyuta.
- kuwepo kwa picha nyingi zenye kuvutia kwa ajili ya kupamba skirini (Backgrounds).
Kabla ya kuanza kutumia windows unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:-
1. Kuhakikisha waya wa umeme umeshaunganisha kwenye kompyuta yako. 2. Kufungua kompyuta kwa kutumia sehemu inayoitwa power. 3. Kusubiri mpaka idhihiri sehemu inayoitwa desktop.
Ndugu msomaji makala hii yenye anuani (hatua za kuendelea kompyuta imeletwa kwenu na ndugu Mahmoudu Twahiri Khamisi mwanafunzi wa chuo kikuu cha Al-zhar nchini Misr kitivo cha maktaba na teknolojia ya habari, naomba usome kwa makini na kama utakuwa unaujuzi zaidi nawe pia unatakiwa kuchangia ili tuweze kuwanufaisha ndugu zetu waswahili nao pia wafaidike na elimu ya kisasa, asanteni sana.