Sayari inaweza kuwa bila mwezi au na miezi mingi. Dunia yetu ina mwezi moja tu. Mshtarii ina miezi zaidi ya 60, mingine mikubwa kama sayari ndogo mingine midogo yenye kipenyo cha 1 km tu. Utaridi haina mwezi.
Mwezi hauna nuru mwenyewe bali kunang'aa jwake kunatokana na nuru ya jua inaoakisiwa usoni mwake kama kwenye kioo.
Mwezi wa Dunia (ardhi) yetu
Mwezi wa dunia yetu ni mkubwa kushinda miezi mingine katika mfumo wa jua. Hakuna jina tofauti kuliko "mwezi" isipokuwa watu wametumia neno la Kilatini "luna" kwa ajili ya mwezi wakitaja mwezi wetu ili kuutofautihsa na miezi ya sayari nyingine.Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja tene uleule tu. Sababu yake ni ya kwamba siku ya mwezi ni sawa na kipindi cha mwezi duniani. Mwezi unazunguka kwenye kipenyo chake katika muda wa siku 27.321 661 za dunia. Upande wa nyuma wa mwezi uko gizani wakati sisi tunaona mwezi mpevu. Wakati kwetu mwezi hauonekani upande wa nyuma unapokea nuru ya jua.
Uso wa mwezi unajaa mashimo ya kasoko yaliyosababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani.
Mwezi (wakati) kama kipimo cha wakati
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamu hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamu tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu.
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ndiyo kalenda ya Kiislamu inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.
Safari kwenda mwezini
Mwezi wetu ni gimba la anga la kwanza ambako wanadamamu wamefika. Tarehe 21 Julai 1969 mwanaanga Mwamerika Neil Armstrong alikuwa mtu wa kwanza wa kukanyaga uso wa mwezi. Waamerika 11 walimfuata katika miaka hadi mwaka 1972. Baadaye safari za kwenda mwezini hazikufanywa tena kutokana na gharama kubwa.Mwezi mali ya watu?
Hata kama Warusi na Waamerika walifikisha mabendera yao mwezini hakuna anayedai mali huko. Katika mkataba wa kimataifa kuhusu anga wa nje nchi 192 za dunia zimepatana ya kwamba mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya bahari. Walipatana pia ya kwamba itakuwa marufuku kupeleka silaha kali kama kinyuklia angani. Mataifa mengi ya dunia yamejiunga na mkataba huo isipokuwa nchi chache hasa za Afrika hazikutia sahihi kama vile Tanzania.Lakini kuna watu binafsi wanaodai mali ya mwezi. Kwanza kuna familia ya Jürgens wanaoishi Westerkappeln (Ujerumani) walipewa hati ya kumiliki mwezi na mfalme wa Prussia Friederich II. tarehe 15.07. 1756 BK. Mfalme alitoa hati kama zawadi ya shukrani kwa huduma bora akiamuru ya kwamba Martin Jürgens atakuwa mwenye mwezi na haki hii itarithiwa na mtoto wa kwanza.
Bila shaka ilhali hakujua haki za mali za Mjerumani katika mwaka 1980 Mwamerika Dennis M. Hope alifika mbele ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akidai mwezi ni wake. Kufuatana na sheria ya Marekani kiwanda ni mali ya mtu akiandikisha dai lake na katika muda wa miaka minane hakuna upingamizi dhidi ya dai lake. Kwa njia hii -iliyowahi kufaulu tayari wakati wa karne zilizopita Wazungu walipojipata Amerika ya Kaskazini (hakuna aliyepinga madai yao mbele ya msajili)- alipata hati ya kumiliki akijaribu kuuza sasa mwezi polepole.