Mwanaanga:Alizaliwa katika familia ya wakulima kwenye jimbo la Ohio
tarehe 5 Agosti 1930. Baada ya kumaliza shule alijiunga na jeshi ambako
alipata mafunzo ya uhandisi na kuwa rubani. 1952 alishiriki katika vita
vya Korea.
Rubani wa majaribio:Mnamo mwaka 1955 aliajiriwa na taasisi ya mambo (shughuli za) (utafiti
wa mambo) ya anga (NASA) kama rubani wa majaribio kwa aina mpya za
ndege. Mnamo mwaka 1958 alikuwa mmojawapo katika kundi la marubani
waliotayarishwa kupelekwa angani.
Mwanaanga:Baada ya kuundwa kwa NASA aliingia katika kundi la wanaanga. Safari yake ya kwanza ilikuwa 16 Machi 1966 kama mwanaanga kiongozi wa Gemini
8. Kilele cha safari hii ilikuwa kukutana kwa Gemini 8 na satelaiti
nyingine na kuunganisha vyombo vyote viwili kwa muda wa masaa kadhaa.
Safari ya kwenda mwezini:Baadaye aliteuliwa kuwa makamu wa kikundi cha wanaanga waliokwenda mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Ajali ya Apollo 1 iliyosababisha kifo cha mwenzake hapo kabla, ndiyo iliyompelekea kujiunga kwake na kundi la Apollo 11. Tar. 20 Julai 1969 Neil Armstrong pamoja Edwin Aldrin
waliutataga uso wa mwezi wakiwa wanadamu wa kwanza mwezini. Walitoka
katika chombo cha angani na kutembea mwezini kwa mara ya kwanza. Picha
hizi zilionyeshwa kote duniani. Akiwa katika hali hii, Armstrong
alitamka maneno yafuatayo: "Hii ni hatua ndogo kwa mtu lakini hatua
kubwa kwa ubinadamu."
Baada ya kurudi salama, Armstrong aliacha kazi katika NASA na badala yake akawa profesa wa uwanaanga kwenye chuo kikuu cha Cincinnati katika mwaka 1971 hadi alipostaafu na kujishugulisha na biashara zake.