Kundi la vijana wa kituruki limekuwa likishindana na kundi la vijana wengine wa Urusi katika kuziteka tovuti mbali mbali duniani.
Mwaka 2005 kundi hilo lilifanikiwa kuziteka computer za vyombo vikubwa vya habari vya marekani kama vile CNN, New York Times, ABD News na vinginevyo na kufanikiwa kutuma virusi kibao ambavyo vilivuruga mitambo yao.
Mojawapo ya tovuti zilizowahi kutekwa na kundi la waturuki ni tovuti ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uraisi wa Marekani kupitia chama cha Republican Duncan Hunter,tovuti ya chama cha soka cha Denmark ,tovuti ya NGO moja ya kupambana na ukimwi nchini Ufaransa ya Solydays.
Katika tukio la jana vijana hao waliwashangaza wadau wa Microsoft waliotembelea tovuti hiyo jumanne asubuhi kwa kukuta meseji ya EID MUBARAK na meseji yao ya kujipongeza kwa kuiteka website hiyo.
Hata hivyo wataalamu wa microsoft walifanikiwa kurekebisha tatizo hilo ingawa liliwachukua masaa kadhaa.
Msemaji wa Microsoft Ireland alisema "Hakukuwa na ubadhirifu wowote uliofanyika kutokana na tukio hilo".
"Kulikuwa na mapungufu katika ulinzi wa tovuti yatu ,Wataalamu wetu wanashughulikia tatizo hili ili lisitokee tena " aliongeza msemaji huyo.
Chanzo: NIFAHAMISHE