Ikionekana
ni kero ama ni unyonyaji kwa wananchi wabunge mbalimbali walipinga
vikali ongezeko la kodi za simu kwani waliona ni kama kumnyonga
mwananchi wa hali ya chini Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, anaandaa maandamano ya amani kupinga tozo ya kodi ya simu kwa wamiliki wa kampuni za simu za mkononi. Mnyika tayari ameshawasilisha barua ya maombi ya maandamano hayo kwa katibu wa Bunge, Job Ndugai Mnyika ameviambia vyombo vya habari kuwa, Julai 15 mwaka huu aliwasilisha barua hiyo ili kufutwa kwa kifungu kinachoidhinisha kampuni hizo kutozwa kodi hiyo. Amesema mpango wake huo umekuja baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013, ambayo imeidhinisha tozo ya kodi za kampuni za simu jambo ambalo litawaathiri wananchi. Hayo yalijulikana wakati wa kuwasilishwa kwa bajeti ya mwaka 2013/14 iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na bajeti hiyo ilifanya marekebisho ya Sheria ya ushuru wa bidhaa na kuanzisha ushuru wa bidhaa kwa kadi za simu kwa mmliki yeyote wa simu za mkononi . Hivyo kufutia tozo hizo wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia maamuzi hayo na kuomba msaada na kuomba na kupendekeza kufanyika kwa maandamano ya kupinga kupitishwa kwa kodi hizo za simu kwa wamiliki wa kampuni za simu kwani kufanya hivyo kutawaathiri watumiaji wa simu za mkononi tozo ambayo imeanza Julai Mosi mwaka huu Amesema ameshaanza hatua ya kukusanya saini za wananchi kupitia mikutano na tayari ameshashasainisha saini zipatazo 23,569 ambazo wamepitisha maandamano hayo. | |||||||||||||||||||||||
Chanzo: NIFAHAMISHE |