Sunday, January 18

Yaya Toure:'Siju hatma yangu Mancity'

Mchezaji nyota katika kilabu ya Manchester City Yaya Toure amesema kuwa hajui hatma yake ya kuichezea kilabu hiyo msimu ujao.
Lakini Meneja Manuel Pelegrini alikuwa wa haraka kufutulia mbali madai ya uhamisho wake akisisitiza kuwa mchezaji huyo wa kiungo cha kati nia yake ni kusalia katika kilabu hiyo.
Yaya Toure ambaye ambaye ametajwa kama mchezaji bora wa bara la Afrika mwaka huu alijiunga na ligi ya Uingereza mnamo mwaka 2010 kutoka Barcelona na amepata mafanikio si haja katika uwanja wa Etihad Stadium.
Lakini katika kipindi cha mwaka uliopita,uhusiano kati ya kilabu hiyo na Yaya si mzuri huku mchezaji huyo akidai kutofurahishwa na hatua ya kilabu hiyo kusahau siku yake ya kuzaliwa.